Wajasiriamali Dar Wapinga Vurugu, Watoa Maazimio Sita Kulinda Amani ya Taifa

 




Na Mwandishi wetu

BAADHI ya wajasiriamali wa kada mbalimbali kutoka wilaya tano za Mkoa wa Dar es Salaam wametoa tamko lenye maazimio sita, ikijumuisha kuwataka Watanzania kujiepusha na vitendo vya vurugu vinavyoweza kuliingiza Taifa katika uvunjifu wa amani.

Tamko limetolewa jijini Dar es Salaam mapema leo Desemba 24,2025 wakati wajasiriamali hao wakizungumza na waziri mkuu wa kiongozi wao na Taasisi ya MECIRA, ambayo imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kutoa elimu ya uraia kwa vijana wadogo.

Wamesema kuwa machafuko hayaleti tija wala suluhu ya kudumu kwa changamoto za gharama na gharama, hofu, hasara za mali na kudorora kwa shughuli za biashara na biashara.



Akisoma tamko hilo kwa niaba ya wajasiriamali hao Suleiman Said mfanyabiashara ndogo kutoka Ilala amesema wanapinga vikali wito wowote unaotolewa na wanaharakati wa ndani na nje ya nchi wanaohamasisha vurugu kwa maslahi binafsi, hali ambayo hupelekea Taifa kuingia katika machafuko na hofu miongoni mwa wananchi.

"Tupo tayari kupaza sauti kupigania ustawi wa Taifa wakisisitiza kuwa bila amani hakuna, ajira ya maendeleo ya biashara na uchumi kwa Watanzania" amesema. 

Amesema Kuwa watawapinga wanasiasa wote wanaotumia vurugu, matusi na amesema uchochezi kama njia ya kutimiza malengo yao Aidha kanuni za demokrasia na maadili ya Taifa.

Pia amesema dhamira yao ya kupinga propaganda zinazotumia kizazi cha Gen-Z kuhalalisha vurugu, fujo na ukosefu wa maadili, huku wakisisitiza kuwa kizazi hicho ni nguvu kazi muhimu na mutakabali wa Taifa.

Naye wajasiriamali Lucy Piter kutoka Tandika amesema amefuatilia matukio ya vurugu yaliyotokea Oktoba 29, 2025 na kubaini kuwafahamu watu nyuma ya pazia wakihamasisha vitendo hivyo.

"Matukio haya yamekuwa somo kwa Watanzania, akisisitiza kuwa uvunjifu wa amani kuleta kuleta maendeleo wala kutoa suluhu ya changamoto zilizopo" amesema. 

Kwa upande wake Hussein Bambe mfanyabiashara kutoka Ubungo amelaani kwa nguvu zote vitendo vya uchochezi na kuwataka vijana wa Kitanzania kutosikiliza watu wanaohamasisha vurugu kwa maslahi ya kisiasa au binafsi.

Amesema wataendelea kupazaficha sauti ya kupinga wanaharakati wanaojihusisha na nchi, wanamitandao wanaoeneza chuki, wanasiasa wanaohamasisha vurugu pamoja na viongozi wa dini wanaoingiza siasa katika majukwaa ya kiimani.



Naye Mzee Omary Suleiman, mfanyabiashara wa Soko la Kinondoni, vurugu hizo zilitokana na uchochezi wa makusudi na kusisitiza kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kuhakikisha matukio kama hayo hayajirudii tena ili Tanzania iendelee kubaki salama, yenye amani na malipo.

Comments