Posts

BRENDA AELEZA MAHUSIANO YA HOTUBA YA LISSU NA GHASIA ZA OKTOBA 29

Image
  SHAHIDI wa utetezi kesi ya uhai inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, Brenda Rupia, amekubaliana na upande wa Serikali kwamba vituo au karatasi za kupigia kura, mali na hata kukata vidole vya waliopiga kura kumaliza uchaguzi au kuwafanya wananchi wengine wasiingie katika mchakato wa kupiga kura. Kauli hiyo ilitolewa Septemba 9, 2026, wakati Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga, akimhoji Brenda katika madodoso yaliyolenga kufafanua maana na athari za msimamo wa kuzuia uchaguzi uliokuwa ukihusishwa na Lissu na CHADEMA kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025. Katuga alimuuliza Brenda kuwa kama vituo vya kuchota karatasi za kupigia kura na kuwa kitendo cha kuzuia uchaguzi, shahidi akajibu, “Ni sahihi.” Alipoulizwa kama majibu mali kuleta kuvuruga amani na hatimaye hatimaye uchaguzi, Brenda pia alikubali. Aidha, alikubali kuwakata vidole vya watu waliopiga kura na kuwatisha wengine wasiende kupiga kura na hivyo kuzuia uchaguzi usifanyike. Katika madodoso hayo, Katuga p...

UDSM YABUNI LISHE KUTOKANA NA MBEGU ZA MCHICHA

Image
  Na Mwandishi wetu  MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Fredrick Pius, amebuni bidhaa ya lishe inayotokana na mbegu za mchicha, akisema zina virutubisho muhimu vinavyoweza kuboresha afya ya watoto na watu wazima. Pius, anayesoma Shahada ya Sayansi ya Chakula na Teknolojia, ameleta ubunifu huo katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea jijini Dodoma, akieleza kuwa imetengenezwa kwa mchanganyiko wa mbegu za mchicha, mbegu za maboga, mtama mweupe na viazi vitamu ili kuongeza thamani ya lishe na kukidhi mahitaji ya makundi mbalimbali ya jamii. "Mbegu za mchicha ndizo malighafi kuu kwa kuwa zina asilimia 14 hadi 17 ya protini zenye amino asidi muhimu ambazo hazipatikani kwa wingi katika nafaka nyingi zinazotumiwa kila siku, hivyo kuzifanya kuwa chakula chenye uwezo mkubwa wa kuboresha lishe"amesema  Amesema bidhaa hiyo pia ina madini ya chuma yanayosaidia kupunguza upungufu wa damu, hasa kwa watoto na wanawake, huku calcium na magnesium vikisaidia ukuaji na uim...

UDSM YABUNI BIDHAA MBALIMBALI KUTOKANA NA MAZAO YA NYUKI

Image
  Na Mwandishi wetu  MWANAFUNZI wa Ndaki ya Sayansi za Kilimo na Teknolojia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Josiana Donald, amebuni bidhaa mbalimbali zinazotokana na mazao ya nyuki, hatua inayolenga kuongeza thamani ya mazao hayo, kutatua changamoto za jamii na kufungua fursa za ajira na biashara. Akizungumza katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea jijini Dodoma, mwanafunzi wa Ndaki ya Sayansi za Kilimo na Teknolojia ya UDSM, Josiana Donald, alisema chuo hicho kinafanya ufugaji wa nyuki wakubwa na nyuki wadogo sambamba na kufanya tafiti zinazowezesha mazao ya nyuki kutumika kuzalisha bidhaa mbalimbali zenye manufaa kwa jamii. Amesema mbali na kuzalisha asali ya nyuki wakubwa na nyuki wadogo, UDSM pia imefanikiwa kutengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo dawa ya kikohozi, dawa ya kung’arisha viatu (Royal Spray Shoe Polish), shower gel na sabuni za mikono zinazotokana na mazao ya nyuki. Kwa mujibu wa Donald, dawa ya kikohozi imetengenezwa kwa kutumia asali ya nyuki wad...

WAZIRI MKUU AAGIZA TADB KUONGEZA UWEZO WA KUFADHILI

Image
  Na Mwandishi wetu WAZIRI Mkuu ameagiza Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kuongeza uwezo wake wa kifedha ili iweze kufadhili kwa kiwango kikubwa zaidi sekta za kilimo, mifugo na uvuvi, akisema hatua hiyo ni muhimu katika kuongeza uzalishaji, kuimarisha usalama wa chakula na kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa. Akizungumza baada ya kutembelea banda la TADB katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea mkoani Dodoma, Waziri Mkuu amesema benki hiyo imeendelea kuwa chombo muhimu cha Serikali katika kuwawezesha wakulima, wafugaji, wavuvi na wawekezaji kupitia utoaji wa mitaji kwa ajili ya shughuli za uzalishaji. Amesema kufikiwa kwa malengo ya taifa ya kuongeza tija katika sekta ya kilimo kunategemea upatikanaji wa mitaji ya kutosha, hivyo kuna umuhimu wa kuendelea kuiwezesha TADB ili ikidhi mahitaji yanayoongezeka ya wadau wa sekta hizo. Amesema kuwa Serikali haiwezi kutegemea ruzuku pekee katika kuendeleza kilimo, hivyo taasisi za kifedha zinapaswa kuwa nguzo muhimu ya uwekeza...

RAIS DKT. MWINYI ASISITIZA KUENDELEZA USHIRIKIANO KWA MASLAHI YA WANANCHI

Image
Na Mwandishi wetu RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano na mawasiliano baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ili kuimarisha na kuendeleza maslahi ya wananchi. Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 30 Julai 2026, alipokutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Ndg. Charles Ngeleja Kadonya, aliyefika kwa mazungumzo ya kikazi kufuatia uteuzi wake katika wadhifa wake mpya. Amesema ushirikiano na mawasiliano yaliyoimarika baina ya pande mbili za Muungano yamechangia kutatuliwa kwa changamoto mbalimbali zilizodumu kwa muda mrefu na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa masuala yenye maslahi ya pamoja. Rais Dkt. Mwinyi ameitaka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuhakikisha Zanzibar inashirikishwa ipasavyo katika majadiliano na mipango ya m...

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO JULAI 30,2026

Image
 

SERIKALI NA WAWEKEZAJI & WATOA HUDUMA MIGODINI WAJADILI CHANGAMOTO NA MAFANIKIO KWENYE SEKTA YA MADINI

Image
▪️Rais Samia apongezwa kwa mazingira rafiki ya uwekezaji ▪️ Wadau wapongeza hatua za serikali za kutatua changamoto ▪️Waziri Mavunde awataka Watanzania kuanza ujenzi wa viwanda vya bidhaa za migodini ▪️ Kampuni ya MANTRA yanuia kuiweka Tanzania kwenye kumi bora ya wazalishaji wa Uranium Duniani Dar es salaam Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa sekta ya madini kupitia majukwaa ya majadiliano kwa lengo la kujenga sekta yenye ushindani, inayovutia uwekezaji na kutoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa Taifa. Mavunde ameyasema hayo katika kikao cha Mining Breakfast Briefing (*MBB*), kilichoandaliwa kwa ushirikiano wa Chemba ya Migodi Tanzania(TCM) na Wizara ya Madini, ambapo ametoa wito kwa wadau kuendelea kutumia majukwaa hayo kujadili fursa na changamoto zinazohusu sekta ya madini. Amewashukuru viongozi na wanachama wa Chemba ya Migodi Tanzania kwa kuendelea kutoa nafasi ya Serikali na wadau kukutana na kujadiliana kuhusu mas...