WAUMINI WAMPELEKA PADRI KITIMA VATIKANI, WAOMBA UCHUNGUZI WA MWENENDO WAKE
Na Mwandishi Wetu
WAUIMINI wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania, Stanslaus Thobias Nyakunga na Elia Phaustine Kabote, wamewasilisha barua kwa Archbishop Angelo Accattino, Balozi wa Vatican nchini, wakiomba uchunguzi wa kichungaji na kiutawala kuhusu mwenendo wa Padri Dkt. Charles Kitima, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC).
Kwa mujibu wa waumini hao, hatua hiyo imechukuliwa kwa malalamiko na mitazamo iliyoenea kwa muda mrefu katika jamii, kwamba Padri Kitima amekuwa akihusishwa na masuala ya siasa za CHADEMA, hususan kuonekana kushiriki katika kushiriki katika chama hicho—jambo ambalo, wanasema, halijaonekana kwa vyama vingine vya siasa.
Waumini hao wanasema mitazamo hiyo, iwe ni ya kweli au la, imeanza kuibua sintofahamu miongoni mwa waumini na kuliweka Kanisa katika mazingira ya uwezekano kama ya upendeleo wa kisiasa, hali inayohatarisha nafasi ya Kanisa kama taasisi ya amani, upatanisho na mwongozo wa kimaadili kwa jamii.
Katika barua yao kwa Balozi wa Vatican, Nyakunga na Kabote wamesisitiza kuwa hawakusudii kutoa hukumu wala kumshambulia mtu binafsi, bali wanaiomba mamlaka ya Kanisa kulishughulikia suala hilo kwa busara ya kichungaji ili kulinda umoja wa waumini na taswira ya Kanisa.
Waumini hao wamerejea pia Maandiko Matakatifu wakisisitiza wajibu wa viongozi wa Kanisa kuwa nguzo za amani na maridhiano, wakinukuu kauli ya Biblia inayosema “Heri wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu” (Mathayo 5:9), pamoja na “Kwa maana Mungu si wa machafuko bali wa amani” (1 Wakorintho 14:33). Aidha, taja onyo la Mtume Paulo dhidi ya mgawanyiko miongoni mwa waumini (1 Wakorintho 1:10).
hiyo ya waumini inakuja katika kipindi ambacho linapitia mjadala mpana wa kisiasa na kijamii, ambapo taasisi za dini zinatarajiwa kuwa na Hatua za kupokea, maridhiano na mshikamano wa kitaifa, badala ya kuonekana kuvutwa katika mvutano wa vyama.
Katika barua yao, waumini hao wameomba mambo matatu makuu: kufanyika kwa uchunguzi wa mwenendo wa Padri Kitima, iliyotolewa kwa mwelekeo wa wazi unaohakikisha uongozi wa Kanisa unabaki huru dhidi ya siasa za vyama, na kuchukuliwa kwa hatua zozotekazolinda umoja wa waumini, amani ya jamii na mamlaka ya kimaadili ya Kanisa.
Waumini wamesema wanaliamini Holy See kuwa na busara na mamlaka ya hao suala linalohusu maslahi mapana ya Kanisa na jamii kwa ujumla.


Comments
Post a Comment