WAZIRI WA NISHATI NDEJEMBI AZINDUA RASMI MITA JANJA


Asema ni mageuzi makubwa ya tekenolojia katika kumuhudumia mteja 

Aelekeza mita hizo kusambazwa katika maeneo yote yenye uhitaji

Na Mwandishi wetu

WAZIRI wa Nishati Deogratius Ndejembi amezindua rasmi mita janja (smart meter) yenye lengo la kuboresha na kumrahisishia mteja kufanya manunuzi ya umemezcC moja kwa moja ikiwa ni maendeleo makubwa ya teknolojia inayofanywa na TAaNESCO katika kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wateja.

Waziri wa Nishati amezindua Mita hizo Disemba 05, 2025 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, wadau wa sekta ya nishati na watendaji wa TANESCO.

Amesema Mita hizo mpya zinamwezesha mteja kupata umeme mara moja baada ya kufanya manunuzi ya ishara bila kutumia kifaa cha ziada cha kuingiza namba (CIU), hatua inayolenga kufikia changamoto zilizokuwa zikijitokeza katika mfumo wa zamani.

“Leo tunajivunia hatua kubwa ya kihistoria zilifanywa na TANESCO ikiwa ni moja ya kampuni ya umma inayofanya vizuri katika utoaji wa huduma kwa wateja nchini" Ndejembi.



Ameongeza kuwa changamoto zilizokuwa zikiwakabili wateja wakati wa kuingiza token ndiyo zimeisukuma Serikali kufanya mageuzi ya kiteknolojia.

“Uzinduzi huu unaweka alama kubwa kwa nchi yetu kwenye mapinduzi ya tekinolojia , hivyo naielekeza TANESCO yote inasamabaza mita hizi maeneo yenye uhitaji mkuwa na kuhakikisha inaendana na vya kimataifa sambamba na kutoa elimu za faida ya mita hizo,” amesisitiza 





Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati,  Salome Makamba, amesema kitengo cha Mita Janja ni mwendelezo wa dhamira ya Serikali katika kuboresha huduma kwa wananchi.

“Nimefurahi kushuhudia hatua hii kubwa ya mapinduzi, ikiwa ni siku ya 33 tangu Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aingie madarakani. Leo tunaweka historia muhimu kupitia ushindi wa Mita Janja kwa wateja wa TANESCO,” alisema  Salome.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chala, amesisitiza umuhimu wa kutetea imani ya umeme na kupongeza TANESCO kwa kuimarisha vyombo vya usalama na usalama katika vitendo vitendo vyao.

“Hatu hii itukumbushe wajibu mkubwa tulionao kulinda. Chalamila.

Aidha, Mkuu wa Wizara ya Nishati, Felichesmi Mramba, ametoa pongezi kwa TANESCO kwa utekelezaji wa Katibu Mkuu, akieleza kuwa teknolojia ya Mita Janja itarasha kwa kiwango kikubwa kikubwa cha changamoto za wateja kabla ya mteja kutoa taarifa TANESCO.



Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO, Balozi Zuhura Bundala, alisema Bodi inaona mageuzi yanayoendelea katika kuboresha huduma zinazotolewa na Shirika na kuwa bodi hiyo inazidi kupata moyo katika kuliongoza shirika linalotoa huduma bora zaidi kidigitali.

Comments