SARANGA YATEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO NDANI YA SIKU 100 ZA RAIS SAMIA.





Na Mwandishi Wetu

DIWANI wa Kata ya Saranga, Eng. John Sanga, amesema kata hiyo imetekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya Afya, Elimu, Maji na Miundombinu ya Barabara ndani ya siku 100 za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwa madarakani.

Eng. Sanga ameyasema hayo leo Januari 28, 2026 jijini Dar es Salaam alisema. Waziri wa habari, ambaye katika sekta ya afya Serikali imetoa shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati itakayohudumia wakazi wa mitaa ya Saranga na Ukombozi.

Amesema ya kusema zahanati hiyo kuweka maabara, wodi za watoto na akina mama wajawazito pamoja na vyoo imekamilika, huku eneo pekee lililobaki likiwa ni la kichomeo taka, hatua ya mwisho kabla ya kuanza huduma kwa wananchi.

Akizungumzia sekta ya maji, Diwani huyo amesema Rais Samia ametoa shilingi milioni 380 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa King'ong'o Water Boosting ambao wamewezesha zaidi ya asilimia 70 ya wakazi wa Mtaa wa King'ong'o kupata huduma ya maji safi na salama, licha ya kuwepo changamoto ndogondogo katika maeneo yenye miiko.




Ameongeza kuwa Rais Samia alimpeleka Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, katika Mtaa wa Ukombozi kutokana na changamoto ya ukosefu wa maji kwa takribani miaka sita, ambapo mradi wa bomba la nchi kumi na mbili kwa sasa upo katika hatua za manunuzi na mkandarasi tayari amepatikana.

Kuhusu barabara, Eng. Sanga amesema Serikali imetoa fedha kwa ajili ya upanuzi wa Barabara ya Morogoro kutoka njia nne hadi sita pamoja na michepuko miwili, hali itakayoongeza njia hadi nane na kunufaisha moja kwa moja wakazi wa Kata ya Saranga.

Amesema pia kata hiyo itanufaika na ujenzi wa Barabara ya Suka–Golani kwa kiwango cha changarawe kama hatua ya muda wa mpango wa DMDP, huku mkandarasi tayari akiwa eneo la mradi akiendelea na kuwekaji wa vifusi, sambamba na Barabara ya Temboni kuelekea Zahanati ya Saranga ambayo tayari ina mkandarasi.

Katika nyingine, Diwani huyo amesema Serikali imeanzisha majukwaa ya wanawake kwa ajili ya utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, ambapo majukwaa hayo tayari yameanzishwa ili kuwawezesha wafadhili kuanza kunufaika na mikopo hiyo.

Akizungumzia suala la ulinzi na usalama, Eng. Sanga amesema ameimarisha ulinzi shirikishi baada ya kukuta changamoto zilizotokana na kuchomwa moto kwa vituo viwili vya polisi wakati maandamano ya Oktoba 29, 2025, ambapo kwa sasa Kata ya Saranga ina mitaa tisa ya kiserikali na kulinda 36 vya ulinzi shirikishi vinavyosimamia usalama wa wananchi mchana na usiku.

Aidha, amesema katika sekta ya elimu kata hiyo ina shule ya msingi na shule tatu za sekondari, ambapo hadi sasa asilimia 75 ya wanafunzi wameripoti shuleni, huku akieleza kuwa makaravati 15 yamesambazwa katika maeneo ya korofi ili kurahisisha wananchi na wanafunzi kuvuka, akisisitiza dhamira yake kuendeleza maendeleo ya kata hiyo.

Comments