CAF KUFANYA MIKUTANO YA KAMATI TANZANIA





Na Mwandishi wetu 

WAZIRI wa Habari, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Patrice Motsepe, ameonesha nia ya kuja nchini Tanzania kwa ajili ya mkutano wa Kamati Tendaji wa shirikisho hilo unaotarajiwa kufanyika Februari 13, 2026, katika Hotel ya Hayat Regency 

Akizungumza na waandishi wa habari, Makonda alisema Januari 16, 2026, Rais Samia alituma ujumbe maalum kwa Rais wa CAF, Patrice Motsepe, kama sehemu ya kutambua mchango wake mkubwa katika kukuza soka Afrika na kuhamasisha amani kupitia michezo.

Makonda amesema kamati tendaji hizo zinatarajiwa kuanza kuwasili nchini kuanzia Februari 10  ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mkutano huo muhimu unaolenga kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya soka barani Afrika.

Amesema ujio wa viongozi hao wa juu wa soka Afrika ni fursa kubwa kwa Tanzania kujitangaza kimataifa kama taifa salama, lenye amani na linalowekeza kwa vitendo katika sekta ya michezo, sambamba na kupata msaada wa kitaalamu na kuhakikisha viwango vya CAF vinazingatiwa kikamilifu.

Kwa mujibu wa Makonda, heshima ya Tanzania katika medani ya kimataifa imeendelea kuimarika kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, hususan katika maendeleo ya mpira wa miguu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Makonda alisema Januari 16, 2026, Rais Samia alituma ujumbe maalum kwa Rais wa CAF, Patrice Motsepe, kama sehemu ya kutambua mchango wake mkubwa katika kukuza soka Afrika na kuhamasisha amani kupitia michezo.

Alisema ujumbe huo uliainisha dhamira ya dhati ya Rais Samia kuendelea kuwekeza katika michezo bila kujali gharama, kwa lengo la kuiwezesha Tanzania kuwa miongoni mwa mataifa makubwa ya soka barani Afrika na hata duniani, hatua iliyompa Motsepe msukumo wa kuimarisha ushirikiano na Tanzania.

Makonda alifafanua kuwa kupitia ushirikiano huo, pande zote zilikutana na kujadiliana masuala mbalimbali, yakiwemo maombi ya CAF kuanza kufanya mikutano yake mikuu nchini Tanzania, jambo lililotokana na kuvutiwa na maendeleo makubwa ya miundombinu ya michezo yaliyopo nchini.

Aliongeza kuwa maandalizi ya mapokezi ya viongozi hao yanaendelea chini ya usimamizi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ili kuhakikisha wageni hao wanapokelewa kwa heshima kuanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa .

Makonda alisisitiza kuwa mafanikio hayo yanapaswa kuendelea kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, akieleza kuwa jitihada zake zimeifanya Tanzania kutambulika kimataifa, kupewa tuzo mbalimbali na kuimarisha diplomasia ya michezo, hatua inayoiweka sekta hiyo miongoni mwa sekta kumi bora zinazochangia maendeleo ya taifa.

Comments