DKT. MWIGULU AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA KUPOOZA UMEME-MKATA
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Mradi wa kupooza umeme uliopo Mkata mkoani Tanga ambao chenye uwezo wa 2X60MVA 132/33kV, pamoja na ujenzi wa njia ya kusambaza umeme wa kilovoti 33 yenye urefu wa kilomita 45 kutoka kituo cha Mkata kwenda kijiji cha Kwamsisi .
Mradi huo unafadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa gharama ya Shilingi Bilioni 44.14 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kupoza umeme na Shilingi Bilioni 5.75 kwa ajili ya ujenzi wa njia ya kusambaza umeme.



Comments
Post a Comment