DKT. MWIGULU AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UMEME-MKATA
Ni ujenzi wa kituo cha kupokea na kusambaza umeme chenye uwezo wa MVA 60.
Mradi kugharimu takribani bilioni 44.
Na Mwandishi wetu
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Februari 12, 2026 amekagua na kuweka jiwe la msingi la Mradi wa ujenzi kituo cha kupokea na kupoza umeme cha MVA 60 Mkatata Tanga na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kilovolti 33.
Akiweka jiwe la msingi mradi huo, Dkt. Mwigulu amesema kutekelezwa kwa mradi huo ni msaada wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania kuhakikisha wananchi wanapata umeme wa uhakika.
"Nitoe rai kwa Wizara ya Nishati kuhakikisha kasi ya ukamilishwaji wa mradi huo unakamilika kwa wakati". Amesisitiza Waziri Mkuu.
Ujenzi wa mradi huo ni shilingi bilioni 44 na unahusisha ujenzi wa vituo viwili vya kupoza na kusambaza umeme uwezo wa MVA 60 kila kimoja kikiwa na MVA 30, pamoja na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kilovoti 33 kutoka kituo cha Mkata hadi kwa Msisi.
“Utekelezaji wa mradi huu unakwenda kuondoa changamoto za umeme katika za Handeni na Kilindi ambazo zinapata kutokea kwa Tanga ambapo ni umbali mrefu”. Amesema Ndejembi.
Amefafanua kuwa kupitia miundombinu hiyo mipya, umeme utasafirishwa kutoka Mkata kwenda Msisi kwa umbali wa kilomita 45, hatua itakayoongeza uwezo wa usambazaji na kuimarisha huduma katika maeneo hayo.
Kuimalika kwa huduma ya umeme Wilaya za Handeni na Kilindi kutachochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii.






Comments
Post a Comment