RC CHALAMILA WAPORAJI ARDHI NA UTAPELI WA AINA YOYOTE DAR KIKAANGONI
Akemea wimbi la utapeli katika Mkoa huo, aitaka Jamii kutokuwa sehemu ya migogoro.
Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ametoa muda wa wiki moja kuanzia leo machi 02, 2026 kwa wahusika wanaojihusisha na vitendo vya utapeli na unyang'anyi wa mali inayohusisha ardhi kujisalimisha kwa kurudisha mali walizozichukua kwa halali kwani Serikali mkoani humo imekusudia kuchukua hatua kali za kisheria kwa wote watakaokiuka agizo hilo.
Kauli hii imekuja kufuatia ziara ya mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es salaam wilaya ya Kinondoni kubaini kukithi kwa vitendo hivyo ambapo baadhi ya watu wanaweza kutumia njia ya kuweka maeneo na baadae kufanya utape.
Chalamila kuongeza kuwa Serikali Mkoani humo pia imebainika kuwepo kwa utapeli show room za kuuzia magari ambapo watu walikuwa wakilipia magari na kudhulumiwa kwa kisingizio kuwa magari yao bado yapo bandarini lakini pia Serikali imebaini uwepo wa mikopo isiyokuwa na tija inayowaumiza wananchi kupitia magumu na kuchukua hatua.
Aidha Chalamila pia ametoa muda wa wiki moja kuanzia Machi 2,2026 akiwataka wananchi wote ambao wanamadai ya kutapeliwa ama Hkudhulumiwa mali zao ikiwemo ardhi kuwasilisha malazklamiko ofisini kwani amekusudia kutekeleza kutekeleza na kutekeleza jukumu hilo kuanzia machi 9 mwaka huu.
Sanjari na hayo Chalamila ameipongeza Mahakama na TAKUKURU kwa namna wanavyoshugulikia kesi huku akitoa tahadhari kwa baadhi ya wasimamizi wa mirathi wanaouza mali za halali kwa kisingizio cha kulea ama kisomesha watoto wa marehemu kwani matukio mengi mengi yametokea kwenye haki zao.
Katika hatua nyingine Chalamila amezungumzia ujio wa Rais Dokta Samia Suluhu Hassan katika Mkoa huo Machi 3, 2026 ambapo anatarajia kuzindua matanki ya kuhifanyia mafuta wilaya ya kigamboni hivyo amewataka wananchi kukitokeza kwa wingi kumuunga mkono Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.




Comments
Post a Comment