TANGA MWENYEJI WA MAADHIMISHO YA KITAIFA YA SIKU YA HAKI ZA MTUMIAJI 2026
- Get link
- X
- Other Apps
MAADHIMISHO ya Kitaifa ya siku ya haki za mtumiaji Duniani kwa mwaka 2026 yanatarajiwa kufanyika Jijini Tanga Machi 15.
Hayo yamebainishwa Jijini Dar es salaam mapema leo Machi 10,2026 na Mwenyekiti wa Jukwaa la watumiaji Tanzania (TCF), na Katibu Mtendaji wa LATRA CCC, Daudi Daudi wakati akizugumza na waandishi wa habari.
Amesema Maadhimisho hayo yanalenga kuhamasisha haki, usalama na ustawi wa watumiaji wa huduma na bidhaa nchini.
" Maadhimisho ya mwaka huu yanaogozwa na kauli mbiu isemayo"Bidhaa Salama Watumiaji wenye kujiamini " na inalenga kuhimiza upatikanaji wa bidhaa na huduma salama zinazozingatia viwango vya ubora ili kuwawezesha watumiaji kufanya maamuzi sahihi na kutumia huduma Kwa kujiamini"amesema
Amefafanua kuwa usalama wa bidhaa na huduma ni msingi muhimu wa kujenga watumiaji wenye kujiamini.
"Watumiaji wenye kujiamini ni wale wanapata bidhaa na huduma salama wanaofahamu haki na wajibu wake, na pia wana uwezo wa kuhoji ubora wa huduma wanazotumia"ameongeza
Aidha amesema katika kuadhimisha siku hiyo TCF itaendesha shughuli mbalimbali za utoaji elimu kwa umma kuanzia Machi 10 hadi 15 mwaka huu ikiwemo vipindi vya uelimishajj kupitia vyombo vya habari pamoja na semina kwa makundi mbalimbali ya watumiaji wa huduma zinazozibitiwa.
Aidha alitoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za Maadhimisho hayo ili kupata elimu kuhusu haki na wajibu wake pamoja na kutumia mifumo iliyopo kutoa maoni au malalamiko kuhusu huduma wanazopokea.
TCF inaundwa na mabaraza ya ushauri ya watumiaji kutoka Mamlaka mbalimbali za udhibiti nchini ambayo ni EWURA CCC, LATRA CCC, TCAA CCC na TCRA CCC.
- Get link
- X
- Other Apps




Comments
Post a Comment