MAADHIMISHO YA MIAKA 19 WRC YAFANA ,VIONGOZI WA DINI, SERIKALI WAHUDHURIA
Na Mwandishi Wetu
VIONGOZI mbalimbali wa dini na Serikali wameungana na waumini leo April 6,2026 kushiriki Maadhimisho ya miaka 19 ya Kanisa la WRC yaliyofanyika Kitunda, Matembele ya Pili jijini Dar es Salaam.
Miongoni mwa viongozi wa dini walioshiriki ni Nabii Boniface Mwamposa , Askofu Joel Bendera, huku upande wa Serikali mgeni rasmi ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Ajira na Mahusiano Deus Sangu, pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpongolo, Mbunge wa Kivule Ojambi Massaburi, Diwani Kivule Rajabu Manyinya pamoja na Mbunge wa Bunda Ester Bulaya.
Maadhimisho hayo yalipambwa na burudani mbalimbali zikiwemo nyimbo za injili kutoka kwa msanii maarufu Rose Muhando pamoja na maigizo yaliyoongeza hamasa kwa washiriki.
Waumini wa kanisa hilo pamoja na wananchi waliohudhuria walionekana kufurahia tukio hilo, wakieleza kuwa limekuwa na mchango mkubwa wa kiroho na kijamii.
Maadhimisho ya miaka 19 ya WRC yameonyesha mshikamano mkubwa kati ya viongozi wa dini, Serikali na jamii kwa ujumla.




Comments
Post a Comment