RAIS DKT. SAMIA ATUNUKIWA TUZO YA KIMATAIFA YA UBINADAMU, UPASUAJI WA UBONGO





Na Mwandishi wetu

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa tuzo maalum ya kimataifa ya Ubinadam ya Upasuaji wa Ubongo, kutokana na mchango wake mkubwa katika kuimarisha sekta ya afya nchini na kimataifa.

Tuzo hiyo imetolewa leo Aprili 16,2026 na Rais wa Chama cha Madaktari wa Upasuaji wa Ubongo Mgongo na mishipa ya fahamu Tanzania Dkt. Othman Kiloloma katika mkutano wa pili wa kimataifa wa Shirikisho la Jumuiya ya Upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu.




Dkt. Kiloloma amesema kwenye taaluma ya upasuaji wa Ubongo, muda ni uhai na mifumo madhubuti ndiyo huamua hatima ya mgonjwa, kupitia uongozi thabiti wa Rais Dkt. Samia Tanzania imeimarisha uwezo wa kukabiliana na magonjwa hatarishi ya ubongo na uti wa mgongo. 




Comments