VITONGOJI VYOTE TANZANIA BARA KUWA NA UMEME IFIKAPO MWAKA 2030- WAZIRI NDEJEMBI
Ataja miradi kadhaa inayotekelezwa na REA
Amshukuru Rais Samia Kinara wa Nishati Safi ya Kupikia
Wabunge waimwagia sifa REA
Bungeni Dodoma
SERIKALI imedhamiria kuhakikisha vitongoji vyote 64,359 vya Tanzania Bara vinafikishiwa umeme ifikapo mwaka 2030 ili kuchochea kasi ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii vitongojini pamoja na utoaji wa huduma bora katika maeneo hayo.
Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi amesema hayo Aprili 22, 2026 Bungeni Jijini Dodoma wakati anawasilisha taarifa ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027 katika Bunge la 13 Mkutano wa Tatu, Kikao cha Kumi na Nne.
“Mwelekeo wa Serikali ni kuhakikisha umeme unafikishwa katika vitongoji vyote Tanzania Bara na ili kufikia azma hiyo, Serikali ilianza utekelezaji wa mradi mkubwa wa kupeleka umeme katika Vitongoji 9,009 ambao utakamilika katika kipindi cha miaka mitatu ijayo,” amesema Waziri Ndejembi.
Amefafanua kuwa miradi inayoendelea kutekelezwa ya kupeleka umeme vitongojini itawezesha vitongoji 50,453 sawa na asilimia 78.4 ya vitongoji vyote vya Tanzania Bara kufikishiwa huduma ya umeme ifikapo mwaka 2028, hatua ambayo itachochea kasi ya ukuaji wa uchumi vitongojini.
Waziri Ndejembi ametaja hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali katika kupeleka nishati vijijini ni kuwa ni pamoja na kuanza utekelezaji wa mradi wa kuongeza uunganishaji wa wateja katika vitongoji (Universal Hamlet Eletrification and Last Mile Customers Connectivity) katika mikoa ya Pwani, Morogoro na Dodoma ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Mahsusi wa Nishati wa Taifa (National Energy Compact) ulioridhiwa katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika (Mission 300) mwezi Januari, 2025.
Hatua nyingine ni utekelezaji wa mradi wa kupeleka umeme katika vitongoji 3,060 sawa na vitongoji 15 kwa kila Jimbo ambao amesema umefikia 80% ya utekelezaji.
“Serikali iliendelea na utekelezaji wa miradi ya kupeleka umeme katika Vitongoji vya Mikoa ya Songwe, Kigoma na Lindi pamoja na maeneo ya migodi midogo ikiwemo wakala wa Nishati vijijini

Comments
Post a Comment