ACT WAZALENDO WAIOMBA SERIKALI IONDOE SH,500 KILA TOZO KATIKA BEI MAFUTA






Na Mwandishi wetu

CHAMA cha ACT Wazalendo kimeishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuondoa kodi ya Tozo ya mafuta kila lita moja watoe shilingi 500 ili kupunguza ukali wa maisha.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana chama cha ACT Wazalendo Abdul  Nondo, wakati wa kuzungumza na Waandishi wa habari kuelezea  kupanda kwa bei ya mafuta nchini kupelekea kupanda kwa gharama za maisha.

"Jumla ya tozo kwenye mafuta Petrol na Dizel lita moja ni shilingi 1,113 tunaishauri Serikali yetu sikivu iondoe kodi na tozo kwa kila lita moja wapunguze shilingi 500 ili kupunguza ukali wa maisha na kupaa kwa bidhaa za vyakula nchini" alisema Nondo.

Mwenyekiti Abdul Nondo, alisema wameshuhudia kuendelea kupanda kwa bei ya mafuta kufikia 4,200 kwa kila lita ambapo alisema ongezeko hilo linapandisha mfumuko wa bei ya bidhaa za vyakula na kupandisha kwa kasi gharama za maisha. 

Aidha alisema kupanda kwa gharama za maisha waathirika wakubwa watanzania wengi wa kipato cha chini na nauli zinapanda na gharama za usafiri zinapanda.

Nondo alisema  ngome ya ACT Wazalendo wanaendelea kusisitiza msimamo wa chama kwamba Serikali ichangie gharama za mwananchi kwa kila lita moja ya mafuta angalu shilingi 400 kama ruzuku ili kupunguza makali ya bei.

Wakati huohuo ACT Wazalendo inatoa pongezi kwa viongozi wote wa chama na wanachama ngazi zote kwa kuadhimisha miaka 12 ya chama cha ACT Wazalendo ambapo kitaifa madhimisho hayo yalifanyika Jimbo la Kilwa Kusini  Mei 05 /2026.

"Tunaposherekea miaka 12 ya ACT Wazalendo chama chetu na ngome ya vijana ACT Wazalendo tunatoa pongezi  maalum kwa kiongozi wa chama Mstaafu Zitto Zuberi Kabwe, kwa kazi kubwa alioifanya kwa kipindi chote cha uongozi wake kazi ambayo inaendelezwa kwa weledi ule ule na kiongozi wa chama aliyeopo sasa madarakani? " alisema.

Comments