UDSM YABUNI LISHE KUTOKANA NA MBEGU ZA MCHICHA

 



Na Mwandishi wetu 

MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Fredrick Pius, amebuni bidhaa ya lishe inayotokana na mbegu za mchicha, akisema zina virutubisho muhimu vinavyoweza kuboresha afya ya watoto na watu wazima.

Pius, anayesoma Shahada ya Sayansi ya Chakula na Teknolojia, ameleta ubunifu huo katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea jijini Dodoma, akieleza kuwa imetengenezwa kwa mchanganyiko wa mbegu za mchicha, mbegu za maboga, mtama mweupe na viazi vitamu ili kuongeza thamani ya lishe na kukidhi mahitaji ya makundi mbalimbali ya jamii.

"Mbegu za mchicha ndizo malighafi kuu kwa kuwa zina asilimia 14 hadi 17 ya protini zenye amino asidi muhimu ambazo hazipatikani kwa wingi katika nafaka nyingi zinazotumiwa kila siku, hivyo kuzifanya kuwa chakula chenye uwezo mkubwa wa kuboresha lishe"amesema 

Amesema bidhaa hiyo pia ina madini ya chuma yanayosaidia kupunguza upungufu wa damu, hasa kwa watoto na wanawake, huku calcium na magnesium vikisaidia ukuaji na uimara wa mifupa.

Pia amesema viazi vitamu huongeza vitamini A kwa ajili ya afya ya macho, wakati mbegu za maboga huchangia protini na mafuta yenye

Amesema ubunifu huo umetokana na kubaini kuwa wafugaji wengi huuza mazao ya nyuki bila kuyaongezea thamani, hali inayopunguza fursa za kuongeza kipato.

Amewataka wananchi na wawekezaji kutembelea banda la UDSM katika Maonesho ya Nane Nane kujifunza kuhusu teknolojia za ufugaji nyuki na fursa zilizopo katika sekta hiyo.

Comments

Popular posts from this blog

AWESO ARIDHISHWA NA WINGI WA MAJI RUVU JUU