RAIS DKT. MWINYI AJIONEA MAFANIKIO YA TANESCO MAONESHO YA SABASABA
Miradi mipya ya kusafirisha umeme kuimarisha upatikanaji wa umeme Zanzibar
Serikali yawekeza Dola za Marekani milioni 282 kuongeza upatikanaji wa umeme na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametembelea banda la Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), ambapo amejionea mafanikio ya utekelezaji wa miradi ya umeme na teknolojia mbalimbali zinazolenga kuboresha huduma kwa wananchi na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Katika ziara hiyo iliyofanyika Julai 13, 2026, Dkt. Mwinyi alipata fursa ya kujionea miradi ya uzalishaji na usafirishaji wa umeme, teknolojia za matumizi bora ya umeme ikiwemo majiko sanifu yanayotumia umeme kwa ufanisi, huduma ya Luku Janja pamoja na mfumo wa Smart House unaomwezesha mtumiaji kufuatilia matumizi ya umeme kupitia simu ya mkononi.
Akitoa maelezo kwa Mhe. Rais, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Lazaro Twange, amesema Serikali inaendelea kutekeleza mpango wa kujenga njia mpya tatu za kusafirisha umeme kutoka Tanzania Bara kwenda Zanzibar kupitia nyaya zitakazopita chini ya bahari.
Ameeleza kuwa njia hizo zitajumuisha Dar es Salaam–Unguja, Tanga–Pemba na Kisiju–Mafia, na kwamba kukamilika kwake kutaongeza upatikanaji wa umeme wa uhakika na uwezo wa kuhudumia ongezeko la mahitaji ya umeme yanayotokana na ukuaji wa viwanda, sekta ya utalii, uwekezaji na shughuli nyingine za kiuchumi visiwani Zanzibar.
Twange amesema Serikali pia inaendelea kutekeleza mradi wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 282, ambapo Dola milioni 6 zimetengwa mahsusi kwa ajili ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa umeme kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO).
“Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa unaoendelea katika sekta ya umeme. Kupitia mradi huu wa Dola za Marekani milioni 282, tunaendelea kuimarisha miundombinu ya umeme, huku sehemu ya fedha hizo ikielekezwa kuhamasisha matumizi ya nishati



Comments
Post a Comment