VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

 


Na Mwandishi wetu

MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imepanga kushirikiana na Kampuni ya Toyota Tanzania Limited ili kuboresha mafunzo ya ufundi magari, hususan kwa wanafunzi wa vyuo vya VETA nchini.

Hayo yamebainishwa  mapema leo Agosti 12,2025 katika ziara ya  Menejimenti ya VETA Makao Makuu ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore, na kuwahusisha Menejimenti na wataalam kutoka VETA Makao Makuu, Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam, Mkuu wa Chuo cha VETA Dar es Salaam na walimu kutoka vyuo vya Dar es Salaam katika Ofisi za karakana za Toyota Tanzania Jijini Dar es salaam 

CPA Kasore amesema lengo la ziara hiyo ni kujifunza kuhusu magari yanayofanywa na Toyota, teknolojia mpya sokoni, na namna inavyowawezesha mafundi kuwa mahiri katika kazi zao. 



Pia amewekaka wazi dhamira ya VETA na Toyota katika kutoa mafunzo ya kusema umahiri kwa wakufunzi na wanafunzi wanaojifunza kupata na magari.

“Magari ya Toyota yanatumika kwa kiwango kikubwa zaidi, hivyo ni muhimu kuwafundisha wanafunzi uelewa wa kina ili wafanye kazi bora wanapoingia kazini,” amesema CPA Kasore.

Meneja Mkuu wa Toyota Tanzania, Kadiva Noah William, ameipongeza VETA kwa hatua hiyo akisema, “VETA tunazalisha tunachotumia (mafundi) na sisi tunatoa huduma mnaitumia (magari na matengenezo), hivyo tunategemeana.”

Kwa upande wake, Mkuu wa Shughuli za Usambazaji wa Toyota, Stanley Joseph, amesema amesema huo utarahisisha utoaji wa mrejesho wa utendaji wa wahitimu wa VETA sambamba na mabadiliko ya teknolojia, pamoja na hayo yanayotumia gesi na mafuta.

Mkufunzi wa Toyota Tanzania, Michael Mruma, ameeleza kuwa kampuni hiyo ina chuo maalum kinachotoa mafunzo ya ufundi na stadi laini kwa mafundi, yakiwemo umakenika, umeme wa magari, urekebishaji bodi, huduma kwa wateja, matumizi ya vifaa na mbinu za Kaizen. 


Amesisitiza umuhimu wa mafundi kuwa na ujuzi wa pamoja wa umakenika na umeme wa magari ili kubaini matatizo kwa haraka, jambo ambalo kwa sasa linatolewa kama fani tofauti katika vyuo vya VETA.

Katika mazungumzo hayo, pande zote ziliona haja ya kurasimisha ili mafunzo yanayotolewa katika vyuo vya ufundi stadi yaendane na uhalisia wa soko la ajira, pamoja na kuinua viwango vya wakufunzi. 

CPA Kasore amesema VETA itaandaa maalum maalum la kurasimisha huo.

Toyota kwa sasa kutoa nafasi za mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa VETA katika vituo vyake vya Dar es Salaam, Tanga na Arusha.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA