WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

 



Na Mwandishi Wetu

WANAFUNZI waliomaliza kidato Cha nne mwaka 1995 katika shule ya sekondari Kidia iliyoko mkoani Kilimanjaro wamechangia zaidi ya sh mil 20 kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa La  Kiinjili La Kiluther Tanzània (KKKT) usharika Wa Kidia.

Wanafunzi  hao wametoa mchango huo kama shukrani na sadaka kwa Mungu kwa kuwawezesha kutumia usharika huo kwa kipindi chote walichosoma shuleni hapo lakini pia wakitumia usharika huo kwa shughuli mbalimbali  ikiwemo za kielimu na kiroho pia.

Mchango huo wa ujenzi pamoja na Zawadi mbalimbali  ambao ni Sadaka ulikabidhiwa  kanisani hapo Agosti 10,2025  katika ibada iliyoongozwa na Mkuu wa pili Wa Jimbo La Kilimanjaro Kati ambaye pia ni Mchungaji Kiongozi Usharika Wa Majengo, ,Mchungaji Israel Moshi,akishirikiana na Mchungaji Kiongozi   Usharika Wa Kidia Mchungaji  Sayuni Shao pamoja na Mchungaji  Kiongozi  Usharika Wa Kirua  Mchungaji James Sambo.

Akizungumza Mwenyekiti wa Umoja Wa Wanawake Wakatoliki Tanzania ( WAWATA) na  RAIS Wa Wanawake Wakatoliki Afrika , ambaye ni miongoni mwa wanafunzi waliomaliza kwa kipindi hicho, Evaline  Malisa Ntenga alisema wanafunzi hao sio kitu bali neema ya Mungu waliyoiita wakati wakimaliza kidato Cha nne mwaka 1995 ndio iliyosababisha kurudi mahali hapo na Kutoa sadaka hiyo.



"Wako wanafunzi wengi waliotamani kufika bali sisi ni  wawakilishi wao," Alisema na kuongeza kuwa ni alama ya shukrani kwa Mungu maana imepita miaka 30 tangu kumaliza kidato Cha nne.

Aidha alisema anashukuru wazazi waliowalea wanafunzi hao na kwamba huo ni wito kwa wazazi nchini Kuwekeza Kwenye malezi.

Aliyekuwa Kaka Mkuu wa shule kwa kipindi hicho,Hendry Kandore alikabidhi majina ya wanafunzi 119 walioanza safari ya  masomo shuleni  hapo kipindi hicho.

Kwa upande wake Mchungaji Moshi  aliwapongeza wanafunzi hao kwa kukumbuka wakati wanasoma na kwamba Uwezo na nguvu za Mungu ziwapiganie katika Maisha Yao kwa Utume waliofanya.



"Tunawapongeza sana, historia mlioacha haitosahaulika kamwe," alisema Mchungaji Moshi huku akiwataka kuendelea kuikumbuka shule ya Sekondari Kidia ambayo bado inaendelea kutoa huduma.

Hata hivyo Mchungaji wa Usharika huo ,Shao  aliipongeza kundi hilo kwa jitijada kubwa walizoonesha Kuichangia  ujenzi wa Kanisa hilo.

" Ni kweli washarika wanaendelea kuongeza juhudi na ujenzi umefikia ngazi ya kuweka madirisha eneo balo hata hawakujua ingekuwaje lakini Mungu amewatumia kutimiza jambo hilo," alisema Mchungaji Shao aliyejawa na furaha wakati wote.

Kundi la wanafunzi hao lilitimiza safari ya miaka minne shuleni hapo mwaka 1995   likijumuisha wanafunzi 119 miongoni mwao wakitoka vijiji tofauti  tofauti  zaidi ya tisa  ambao walitumia muda mrefu kutembea kwa ajili ya kuisaka elimu na kufanikiwa kuwa katika taaluma mbalimbali nchini.

Comments

Popular posts from this blog

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA