MAWAZIRI WA NISHATI JUMUIYA YA SADC KUKUTANA NCHINI ZIMBABWE.
Masuala ya Umeme, Gesi, Nishati Safifawa
Na Mwandishi wetu
KAMISHNA wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga ameongoza kazi ya Wataalam kutoka Wizara ya Nishati katika Kikao cha awali cha Kamati Ndogo ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kilicholenga maandalizi ya Mkutano wa Pamoja wa Kamati ya Mawaziri wa SADC wanaoshughulikia masuala ya Nishati itakayofanyika nchini Zimbabwe.
Kikao hicho cha awali kimefanyika Mei 30, 2025 katika Ukumbi wa Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam kwa njia ya mtandao.
Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa SADC unatarajia kufanyika nchini Zimbabwe Mei 30 had 04 Juni 2025 ukiongozwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Nishati wa SADC.
Kikao hicho cha Mawaziri kitajadili agenda mbalimbali katika hali ya upatikanaji wa umeme katika Kanda; Maendeleo ya sekta ndogo ya Mafuta na Gesi, Matumizi ya Nishati Safi na nafasi na utayari wa Kanda katika kutekeleza Azimio la Dar es Salaam lililotokana na Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Misheni 300.
Washiriki wengine katika kikao hicho kilichofanyika kwa njia ya mtandao wametoka katika nchi zote zilizopo katika Jumuiya ya SADC.



Comments
Post a Comment