SALUM : WATANZANIA TUMUUNGE MKONO RAIS DKT SAMIA KWA MAZURI ALIYOYAFANYA

 




Na Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM 

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa UVCCM Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dodoma Salum Ismaili Salum amewaomba.
watanzania kumuunga mkono Rais Dkt Samia kutokana na mazuri aliyofanya katika Uongozi wake .

Salumu ametoa wito huo Jijini Dar es Salaam mapema leo Juni 18,2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo kutagaza nia ya kugombea ubunge katika Jimbo la Kahama Mjini Mkoani Shinyanga .

Amesema Rais Dkt Samia Wakati anapokea kijiti Cha uongozi baada ya kifo cha Rais Dkt. John Magufuli na miradi mingi ambayo ilikuwa ikiendelea.




"Kutokana na Mazingira haya watu wengi walidhani Rais Samia asingeweza kuiendelea na kuikamilisha, hivyo ameitekeleza vizuri na kuikamilisha jambo ambalo linafanya Watanzania wamuunge mkono"amesema 

Aidha amekemea watu wanaomkejeli na kumsema vibaya kwamba hawatawavumilia.

Akizungumzia kuhusu Nia ya kugombea ubunge Jimbo la Kahama Mjini Mkoani Shinyanga amesema kugombea kwa sababu Rais Samia ambeya ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ametoa fursa ya uongozi kwa vijana.

"Nimeamua kutagaza nia ya kugombea ni kwa ajili ya kuwaletea maendeleo Wananchi wa Kibaha mjini kwani kupitia fursa nyingi zilizopo jimboni humo ikijumuisha madini ya Madini"amesema 

Amesema Juni 28 Mwaka huu atakuwa ni miongoni mwa watakaojitokeza kuchukua fomu.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA