CHALAMILA AKOSHWA HUDUMA ZA TANESCO,ATAKA WENYEVITI KUELEZA, KULINDA MIUNDOMBINU
Na Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amewataka wenyeviti wote kuwa mabalozi wa kueleza huduma nzuri zinazotolewa na Shirika la umeme Tanzania (Tanesco ) pamoja na kulinda miundombinu ya Shirika hilo.
Chalamila ameyabainisha hayo mapema leo Juni 24, 2025 wakati akifungua kikao kazi kati ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na wenyeviti wa serikali za mitaa kutoka Wilaya ya Kinondoni na Ubungo.
Amesema Wenyeviti ni miongoni mwa wadau muhimu wa kulinda miundombinu ya Tanesco, utekelezaji wa miradi ya shirika hili upo kwenye ngazi ya mitaa ambayo inaongozwa na wao
"Wenyeviti wa Serikali za mitaa ninyi ni wadau muhimu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Serikali ikiwemo ya Tanesco kwa kuwa miradi hutekelezwa katika maeneo yane ya kiutawala.
Aidha ameipongeza Tanesco kwa kuona umuhimu wa kukutana na kundi hilo muhimu ili liweze kufahamu kwa kina majukumu ya shirika hilo .
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco,Lazaro Twange amesema shirika hilo limeona upo umuhimu wa kukutana na Wenyeviti wa Serikali za mitaa kutokana na kuwa ni wadau muhimu katika jamii.
"Kikao kazi hiki ni kwa ajili ya ya kutengeneza mfumo mzuri wa mawasiliano ambao utatusaidia kujua wananchi wanasemaje kuhusu huduma za Tanesco sambamba na kutoa elimu ya uelewa ambao watautumia kuelimisha jamii,"amesema.





Comments
Post a Comment