CHODAWU YAWAKUMBUKA WATOTO WACHANGA HOSPITALI YA AMANA

 





Na Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM 

CHAMA cha Wafanyakazi Majumbani (CHODAWU),kimeungana na watu mbalimbali duniani kuadhimisha siku ya Wafanyakazi Duniani ambapo kila  mwaka Juni 16 mataifa mbalimbali  uadhimisha siku hiyo.

CHADAWU katika kuadhimisha siku hiyo imetembelea Hospitali ya Amana katika wodi ya watoto wachanga na kutoa msaada wa vitu mbalimbali ambavyo vitawasaidia  watoto hao.


Akizungumza  jijini Dar es Salaam, mapema leo Juni 16,2025  Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Majumbani, Zanini Athuman, wakati wa kukabidhi msaada huo wakishirikiana na 

Shirika la Kazi la Kimataifa(ILO) nchini amesema katika kusherehekea siku hiyo wameiomba  Serikali na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuridhia Mkataba wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Namba 189, unaohusu kazi zenye heshima kwa wafanyakazi wa majumbani.



Amesema  Wafanyakazi wa majumbani wana umuhimu wao mkubwa katika jamii na changamoto nyingi wanazokabiliana nazo, huku wakisisitiza kuwa nyumba za waajiri wao zinapaswa kutambuliwa rasmi kama Ofisi zao.

Athuman  amesema wafanyakazi hao kwa muda mrefu wamekuwa wakinyanyasika kwa kubakwa,kupigwa,kutakiwa kimapenzi na wenye nyumba na wengine kutolipwa stahiki zao huku kukiwa hakuna wa kuwasema.

"Sisi tuna mchango mkubwa sana katika jamii na vile vile tunaongeza kipato katika nchi.



" Uwepo wetu huwezesha viongozi kama wabunge, mawaziri, watumishi wengine wa serikali, na akina mama wafanyabiashara kwenda kutekeleza majukumu yao huku wakijua kuwa nyumba zao na familia zao zimetunzwa na sisi ambao tunakuwa walimu,walinzi na pia wazazi katika nyumba ,zao,"amesema

Akizungumzia msaada waliokabidhi kwa watoto hao amesema wameguswa kwa kuwa asilimia kubwa ambao wamekuwa wakiwahudumia majumbani ni watoto na kina mama,hivyo wameona waonyeshe upendo huo kwao katika siku hii ya wafanyakazi majumbani.

Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa kuboresha ufanyaji kazi mahala pa kazi kwa wafanyakazi majumbani kutoka Shirika la Kazi la Kimataifa(ILO),Chiku Khamis, amesema majumbani ni sehemu ya kazi kwa wafanyakazi hao hivyo ni vema wakaheshimiwa na kuthaminiwa kama wafanyakazi wengine.

"Tunashukuru Chodawu kutualika kuwa pamoja nao katika siku ya leo,siku ya leo ni siku ambayo mkataba wa kitaifa 189 uliridhiea mjini Geneva na mkaya huu ulikuja baada ya kuona wafanyakazi wa majumbani ni wafanyakazi kama wengine lakini kuna haki na stahiki zao hawazipati.

Amesema mkataba huu uliundwa ili kuhakikisha kazi zenye staha kwaajili ya wafanyakazi wa majumbani ndio walezi na wameonesha umoja wao leo kuja hospitalini na kuleta vifaa kwaajili ya mama na watoto kuonesha kiasi gani wao ni walezi na wanajali familia zetu,"alisema.

Naye  Msimamizi wa wodi ya watoto, Mary Machema, aliwashukuru Chodawu kwa msaada wao  na kueleza utawasaidia katika kuwahudumia watoto hao ambao wengine wazazi wao hawana uwezo na wengine hawana wazazi kabisa.

Mary amesema wodi hiyo imekuwa ikipokea watoto wachanga wenye matatizo mbalimbali yakiwemo ya upumuaji, kuzaliwa na uzito mdogo au kupata maambukizi wakati na baada ya kuzaliwa.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA