DKT. MPANGO ATEMBELEA KAMPUNI YA KIMATAIFA YA UZALISHAJI VIFAA TIBA






Na Mwandishi wetu

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango ametembelea Kampuni ya Kimataifa ya Uzalishaji Bidhaa za Tiba ya Health 3000 iliyopo Roma nchini Italia Juni 23, 2025.

Makamu wa Rais amefanya mazungumzo na viongozi wa kampuni hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kampuni hiyo Maurizio Flammini pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni Eleonora Flammini.



Mazungumzo hayo yamelenga ushirikiano baina ya Tanzania na Kampuni ya Health 3000 hususani katika matibabu kwa njia ya mtandao (Telemedicine).

Kampuni hiyo ni moja ya Makampuni yaliyo chini ya mwamvuli wa FG Group ambayo imejikita katika kutoa huduma za afya hususani vifaa vya kutumia teknolojia ya teknolojia ya kisasa.




Makamu wa Rais yupo nchini Italia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Ubia wa Maendeleo kati ya Afrika na Serikali ya Italia (Mattei Plan) pamoja na mikutano mbalimbali ya uwili.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA