ELIMU KUHUSU OWM SERA,BUNGE NA URATIBU KUENDELEA KUTOLEWA

 



Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI wa Idara ya Uwezeshaji Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi Conrad Milinga amesema, maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yamewezesha Ofisi ya Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) kutoa elimu juu ya fursa mbalimbali za kupokea mikopo na mifuko ambayo iko katika sekta mbalimbali na uwezeshaji wananchi kifedha.

Milinga ametoa kauli hiyo Juni, 23,2025 wakati wa kilele cha Maadhimisho Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika katika viwanja vya Chinangali park Jijini Dodoma.

 


Amesema Ofisi ya waziri Mkuu imetumia taarifa ya wiki hiyo kueleza wananchi na wadau mbalimbali kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na ofisi hiyo ikiwa ni Uwezeshaji wananchi kiuchumi, namba ya kujinginga na maafa na alama za taifa ambazo ni Wimbo wa Taifa, Ngao ya Taifa na Bendera ya Taifa.




 

“Tumeweza kuelimisha wananchi kuhusu unaotumiwa na Idara ya Menejimenti ya Maafa unaoweza kutambua majanga mapema hayajatoke ili kuwapa wananchi tahadhari ya kujiandaa kabla hayo majanga hayajatokea, tumetoa uelewa kwa wananchi kuweza kufahamu maatumizi sahihi ya alama za taifa ikiwa ni sahihi ya taifa , beti za wimbo wa Taifa ambapo wimbo huo unatakiwa kuimbwa beti zote mbili za Taifa, sahihi.

 

Aidha, ameongeza kuwa , ofisi imeweza kutoa elimu kwa umma kuhusu Idara ya Ufutiliaji na Tathimini ya shughuli za serikali inavyohusika katika kutoa taarifa za utekelezaji wa miradi mabalimbali inayotekelezwa hapa nchini.




 

 

Mbali na hayo, Mkurugenzi Milinga ametoa wito kwa wananchi kujitokeza katika Maonesho ya Kimataifa ya Sababa ambapo Ofisi ya Waziri Mkuu itashiriki maonesho yanayotarajiwa kuanza tarehe 28 Juni, 2025 Jijini Dar Es Salaam.

 “Katika maonesho hayo Ofisi ya Waziri Mkuu kwa taasisi na taasisi zote itachangia kushiriki katika kutembelea maonesho hayo ili kupata elimu kuhusu shughuli zote zinazofanya na Ofisi ya Waziri Mkuu.




 

Madhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yalianza tarehe 16 Juni, 2025 hadi tarehe 23 Juni, 2025 chini ya kauli mbiu isemayo “Himiza Matumizi ya Mifumo ya Kidigiti ili Kuongeza Upatikanaji wa Taarifa na Kuchagiza Uwajibikaji”

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA