ETDCO YANG'ARA TUZO SEKTA YA UJENZI



Na Mwandishi wetu

KAMPUNI ya Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme (ETDCO) imefanikiwa kupata Tuzo ya heshima ya Mkandarasi Bora wa Ujenzi na Miundombinu ya Umeme pamoja na mifumo ya kampuni kutoka Construction Times Gala and Award 2025 zilizofanyika 28 Juni 2025, jijini Dar es Salaam.

Katika tuzo hizo, Kaimu Meneja Mkuu wa ETDCO, CPA Sadock Mugendi, pia ametunukiwa Tuzo ya Uongozi Bora katika Uendeshaji wa Kampuni, ikiwa ni mchango wake katika kufanikisha miradi.


Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo hizo, iliyokwenda sambamba na kampuni ya Jarida la Ujenzi, Afisa Uwekezaji Mwandamizi wa TIC, Gaudence Nicholaus Mmassy, amepongeza washindi wote kwa mchango wao mkubwa katika maendeleo ya sekta ya ujenzi nchini.



Alisema alipopokea hizo Kwa niaba ya Kaimu Meneja Mkuu wa ETDCO, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa Kampuni ya ETDCO, Mhandisi Dismas Masawe, amesema kuwa tuzo hizo ni uthibitisho wa kutambua mchango mkubwa wa kampuni ujenzi wa tuzo ya umeme nchini kwa kuonesha dira ya maendeleo katika kufuatilia utekelezaji wa majukumu yao.

“Siri ya mafanikio haya ni thabiti kutoka kwa menejimenti ya Kampuni, pamoja na kujitolea kwa dhati kwa utekelezaji wetu, utekelezaji wa Miradi kwa weledi wa hali ya juu.” amesema Mhandisi Masawe.

Katika tuzo hizo za heshima zilizotolewa na Construction Times, jumla ya jumla nane yalitunukiwa tuzo hizo za heshima, huku ETD ikijivunia kuondoka na tuzo mbili kubwa kutokana na utendaji wake bora, hasa katika suala la Miradi na kimsimamo ya Kampuni.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA