KAMISHNA WA UMEME NA NISHATI JADIDIFU AFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI YA UMEME JIJINI DAR ES SALAAM
Aridhishwa na hatua ya utekelezaji wa miradi
Awataka wakandarasi kuzingatia sheria na TANESCO kutuma maombi ili kuondoa gharama
Aisisitiza dhamira ya Serikali ya kuhakikisha Watanzania wanapata umeme wa uhakika
Na Agnes Njaala, Dar es Salaam
KAMSHNA wa Umeme na Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga, Juni, 12 2025, amefanya ziara ya kukagua miradi ya umeme ya Gridi Imara Imara inayoendelea Jiji la Dar es Salaam, na kutoa maelekezo muhimu kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) pamoja na wakandarasi wanaotekeleza mradi huo.
Miradi hiyo inalenga kupata upatikanaji wa umeme kwa kuboresha ya usafirishaji na kutuma umeme katika nchi, ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa huduma bora na uhakika kwa wananchi.
Akizungumza mara baada ya ziara hiyo, Kamishna amesema ameridhishwa na hatua zilizofikiwa katika miradi hiyo, licha ya changamoto mbalimbali za kimazingira, na kusisitiza umuhimu wa kuendelea na kutekeleza miradi inakamilika kwa wakati.
“Nimeridhishwa na hatua zilizofikiwa, lakini nimeagiza wakandarasi waharakishe kazi, vifaa vipatikane kwa wakati, viwango vya kazi vizingatiwe ili miradi hii itoe matokeo yaliyokusudiwa kwa wananchi,” amesisitiza Mhandisi Luoga.
Akifafanua amebainisha kuwa miradi hiyo ya kimkakati, inayotekelezwa na TANESCO kwa ufadhili wa Serikali, inalenga kuboresha huduma ya umeme kwa wakazi wa Dar es Salaam na maeneo mengine nchini.
Aidha, ametoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuidhinisha fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo muhimu.
Katika maagizo yake, ameitaka TANESCO kuongeza matumizi kwa wakandarasi katika upatikanaji wa vifaa kwa wakati, ubora wa kazi ili kuepuka gharama zitokanazo na ucheleweshaji.
Kwa upande wake, Mhandisi Abdallah Chikoyo, Meneja wa Miradi ya Kuzalisha Umeme TANESCO aliyemwakilisha Mkurugenzi , ameahidi kuongeza juhudi wakati miradi na kuweka mipango kazi inayotekelezeka kwa wakati.
“Tumejipanga kuongeza nguvu katika miradi hii, na kuendelea na wadau wa maendeleo ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na ufanisi, tukitimiza wajibu katika kuboresha huduma ya umeme,” amesema Mhandisi Chikoyo.
Ziara hiyo ilikua sehemu ya utekelezaji wa wajibu wa Serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ambapo Kamishna Luoga alitembelea vituo vya umeme vya Ubungo I, Mabibo, Kinyerezi na Gongo la Mboto. Katika vituo, kazi ya ufungaji wa mashine ukiwa na uwezo mkubwa (transformers) inaendelea kwa kasi ya kuridhisha, ikiwa ni hatua ya kupata mafanikio ya umeme jijini Dar es Salaam.




Comments
Post a Comment