MAKALLA: THE ROYAL TOUR IMEKUZA UTALII KASKAZINI
Na Mwandishi wetu ,BABATI
KATIBU wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi an Mafunzo wa chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla amesema Rais Samia Suluhu Hassan amefanya jambo kubwa katika mikoa ya Kaskazini kwa kukuza utalii kupitia filamu ya The Royal tour.
Amesema kupitia filamu hiyo sekta ya utalii imeimarika kwani imesaidia kuutangaza utalii uliopo nchini katika mataifa mbalimbali ambayo imechangia kuongeza mapato katika sekta hiyo na wananchi wa Mkoa wa Manyara ni moja ya wanufaika wake.
Makalla ameyasema hayo leo Juni 4,2025 wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Mollel Papaa katika Wilaya ya Babati Mkoani Manyara akianza ziara yake ya siku tisa katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara.
Makalla amesema watalii wanapoingia kwa wingi nchini mapato yanaongezeka kutokana na kuongezeka kwa mzunguko wa fedha na yote hayo ni kutokana na ubunifu wa Rais Samia wa kufikiria kuitangaza Tanzania kupitia Filamu hiyo ambayo wananufaika kwa sasa.
“Kikubwa kilichofanyika katika mikoa ya kaskazini ni kukuza utalii kupitia ‘The Royal tour’ imefanya kazi kubwa katika mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro kwani mapato ya utalii yameongezeka na nyie Manyara mnafaidiaka nao kwani mpo karibu na Karatu, Tarangire na Mbuga ya Manyara,” amesema Makalla
Makalla amesema Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye, ameeleza kwa kirefu juu ya serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia akihusisha historia ya Tanzania tangu kuasisiwa kwake na inapoelekea ambayo maingi wake unawekwa na Rais Samia.




Comments
Post a Comment