NAIBU WAZIRI KHAMIS AWATAKA WANANCHI KUPANDA MITI



Na Mwandishi wetu

NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Khamis Hamza Khamis ametoa rai kwa wadau wa mazingira katika ngazi zote na wananchi kwa ujumla kuungana na Serikali kwa hali na mali katika mapambano dhidi ya kuenea kwa hali ya jangwa na ukame kwa faida ya vizazi vilivyopo na vijavyo. 

Pia, amewaomba wananchi kuendelea kupanda miti na kuitunza ili kukabiliana na athari za ukame ambao unaathiri sekta mbalimbali ikiwemo maji, mifugo na kilimo ambazo zina umuhimu mkubwa kwa binadamu. 




Ametoa wito huo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Kuenea kwa Hali ya Jangwa na Ukame Duniani yaliyofanyika kitaifa Juni,17 2025 katika Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza na viongozi na wananchi,  Khamis amesema pamoja na mambo mbalimbali Tanzania pamoja na jumuiya za kimataifa kwa kushirikisha vizazi vilivyopo na vijavyo, imejitolea kuongoa hekta bilioni moja ya ardhi iliyoharibika kufikia mwaka 2030.




Amesema Tanzania ni moja ya waathirika wa hali ya ukame hivyo Serikali imechukua hatua mbalimbali kuhakikisha inakabiliana na tatizo hilo kwa ufanisi mkubwa kwa kushirikisha wizara za kisekta, taasisi za umma, washiriki wa maendeleo, mashirika yasiyo ya kiserikali, sekta binafsi na taasisi za kidini.




Halikadhalika, Naibu Waziri Khamis amebainisha kuwa Serikali imeandaa Mpango wa Kitaifa wa Kupambana na Kuenea kwa Hali ya Jangwa na Ukame, imefanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Mazingira.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA