SERIKALI IMENUFAIKA KWA KIASI KIKUBWA NA FEDHA ZA MRADI MABADILIKO YA TABIA YA NCHI - WAZIRI MASAUNI.
- Get link
- X
- Other Apps
Na Mwandishi wetu.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi muungano (Muungano na Mazingira) Hamad Masauni amesema Serikali ya Tanzania imenufaika kwa kiasi kikubwa na fedha za mradi wa mabadiliko na mabadiliko ya mradi, mapato na ushawishi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika majukwaa ya kimataifa.
Akizungumza mbele ya wananchi wa Bariadi Juni 18, 2025 wakati wa mkutano wa hadhara wa majumuisho ya ziara ya Rais Samia mkoani Simiyu, Masauni amesema kuwa athari za mabadiliko ya tabianchi kama ukame, mafuriko na uoto wa historia zinatokana na Nchi zinazoendelea.
“Mhe Rais, moja ya matunda ya juhudi zako ni utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji unaogharimu zaidi ya Euro milioni 313, ambao kesho tutaenda kuutembelea. Huu ni ushahidi kuwa uongozi wako umeleta mabadiliko chanya katika changamoto na changamoto za mabadiliko ya tabianchi,” amesema Masauni.
"Mheshimiwa Rais nipende kukupongeza wewe binafsi tangu ukiwa Makamu wa Rais ulipambana athari hizi za Mabadiliko ya tabianchi ambazo vyanzo vyake ni nchi zilizoendelea kama nchi yetu tunanufaika na fursa zinazojitokeza.
Pamoja na suala la mazingira Waziri Masauni amezungumzia matunda ya Muungano ambapo ameeleza watu wengine wa bara wanaishi Zanzibar kama ilivyo kwa watu wa Zanznibar ambao huishi Bara.
"Watu wenye asili ya usukuma wapo Zanzibar na watu wenye asili ya Zanzibar wapo Simiyu."
- Get link
- X
- Other Apps



Comments
Post a Comment