TANESCO YAJA NA KAMPENI YA "LIPA DENI,LINDA MIUNDOMBINU, TUKUHUDUMIE



Na Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM 

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) imezindua Kampeni maalum ya "Lipa Deni, Linda Miundombinu, Tukuhudumie yenye lengo la kuhamasisha ulipaji wa madeni kutoka kwa wateja wa malipo ya baada na ukaguzi wa mita za Luku kwa wateja wa malipo kabla.

Akizugumza na waandishi wa habari mapema leo Juni 19, 2025 Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma TANESCO Irene Gowelle amesema kampeni hiyo imeanza leo Juni 19 , 2025 na itaenda sambamba na kauli mbinu isemayo “Huduma endelevu huanza na wewe”.

"Zoezi  hili la kampeni litaenda sambamba na kuhamasisha ulinzi wa miundombinu ya umeme ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha na kuimarisha uendelevu wa upatikanaji wa huduma bora ya umeme kwa wananchi"amesema Gowelle 

Akitaja malengo ya kampeni hiyo amesema imelenga  kuwahamasisha wateja wa malipo ya baada ya kulipa madeni yao kwa hiyari kabla ya hatua za kisheria kuchukuliwa.




Pia amesema kampeni hiyo itatoa motisha kwa ulipaji wa wakati ikiwemo msamaha wa riba kwa wateja watakaolipa madeni yao kikamilifu.

"Kampeni hii itahusisha ukaguzi wa mita za luku kwa lengo la kuhakikisha zinafanya kazi vizuri na hazijachezewa na wateja wasio waaminifu"amesisitiza Gowelle 

Aidha amesema Kupitia kampeni hiyo watahamasisha umuhimu wa ulinzi shirikishi wa miundombinu ya umeme kwa kuwajumuisha wananchi na kuwapa elimu ya kulinda miundombinu ya shirika.

Katika hatua nyingine Gowelle alitoa wito  wateja wote nchini ambao wanadaiwa kutoa ushirikiano kwa kulipa madeni yao kwa wakati na hivyo kutoathiri upatikanaji wa huduma ya umeme kwenye shughuli zao.

Mwisho 

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA