TANESCO YASHINDA TUZO YA UHIFADHI WA MAZINGIRA KUPITIA MRADI WA JNHPP.
Na Mwandishi wetu, DODOMA
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limekabidhiwa tuzo ya uhifadhi wa mazingira katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Kitaifa yaliyofanyika jijini Dodoma mapema leo Juni, 5 2025.
Tuzo hiyo imetoa mchango wa TANESCO katika kuhifadhi mazingira kupitia utekelezaji wa Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), umeendelea kuzingatia misingi ya utunzaji wa mazingira sambamba na kuchangia gesi joto.
Tuzo hiyo ilitolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, na kupokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Lazaro Twange, katika hafla rasmi rasmi hayo.
Kupitia ushiriki wake katika maonesho hayo, TANESCO imeendelea kuonesha dhamira ya dhati ya kutekeleza miradi mikubwa ya umeme kwa usalama wa mazingira, ikiwa ni pamoja na JNHPP na mingineyo inayolenga kuleta manufaa kwa vizazi vya sasa na vijavyo.


Comments
Post a Comment