TFS YAWAVUTIA WANANCHI DODOMA KWA TIBA YA NYUKI KWENYE WIKI YA MAZINGIRA

 



Na Mwandishi Wetu, DODOMA 

MAMIA ya wananchi wamejitokeza katika bendi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kupata huduma mbalimbali za kielimu na kiafya wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Duniani yanayoendelea jijini Dodoma.

Miongoni mwa vivutio katika banda hilo lililoko viwanja vya Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC), ni huduma ya tiba ya kuimarisha kinga ya mwili kwa kutumia nyuki (api-therapy), iliyokuwa ikitolewa na Mhifadhi Brenda Mwakipesile kutoka TFS.

Mwakipesile amesema tiba hiyo ya asili kungojea kinga ya mwili na kutoa ahueni kwa baadhi ya maumivu ya muda mrefu, hasa ya viungo.




“Tiba hii hutumia sumu ya nyuki kwa njia ya salama na inayodhibitiwa, na imekuwa na matokeo chanya kwa baadhi ya wagonjwa waliowahi kuipokea.

Mbali na huduma hiyo, TFS ilitoa elimu kwa wananchi kuhusu uhifadhi wa misitu, matumizi ya nishati safi ya kupikia, kuweka wa mkaa mbadala, upandaji wa miti na utunzaji wa vyanzo vya maji.

Maonesho haya yamebebambiu: “Mazingira Yetu na Tanzania Ijayo, Tuwajibike Sasa – Dhibiti Matumizi ya Plastiki”, yakihusisha taasisi za serikali mbalimbali, mashirika ya kimataifa, sekta binafsi na wananchi.




Wananchi waliotembelea banda la TFS walionesha kufurahishwa na huduma na elimu waliyoipata, wakieleza kuwa ni tofauti na ilivyozoeleka katika maonyesho mengine.

“Nimejifunza mengi kuhusu misitu, lakini pia sikuwahi wakatiwahi nyuki ungana kama tiba. Ni jambo jipya na la kuvutia sana,” alisema Rehema John, mkazi wa Dodoma.

Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira yanatarajiwa kuona kilele chake Juni 5, yakilenga kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira kwa mustakabali wa Taifa.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA