WAZIRI MKUU MAJALIWA KUZINDUA KAMPENI YA MAMA SAMIA LEGAL AID



Na Mwandishi wetu.

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Kampeni ya Mama Samia Legal Aid inayotarajia kufanyika Juni 16, mwaka huu katika viwanja vya Maturubali Mbangala Jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam mapema leo Juni 13, 2025  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amesema lengo la kampeni hiyo ni kuimarisha upatikanaji wa haki kwa wananchi.

“Nawaoba wakazi wa Mkoa  Dar es Salaam mjitokeze kwa  wingi siku ya uzinduzi wa kampeni hii na baadaye itaendelea katika Halmashauri zote za Mkoa huu,”kwani dhamira ya Serikali  ni kuhakikisha inatatua matatizo katika jamii amesema Chalamila.

Amesema kampeni hiyo itafanyika kwa muda wa siku tisa mfululizo na itajikita katika kutoa huduma za  usaidizi wa kisheria kuhusu mirathi, migogoro ya ardhi, masuala ya ndoa, uandishi wa wosia, na huduma nyingine za kisheria zitakazotolewa na wataalamu wa sheria waliobobea.

Aidha aliwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kunufaika na huduma hizo zitakazokuwa zikitolewa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa kipindi chote cha kampeni.





Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Ester Msambazi, amesema kuwa kampeni hii inalenga kusaidia wananchi wenye kipato cha chini ambao wamekuwa wakikosa huduma za kisheria kutokana na changamoto za kiuchumi na uelewa mdogo kuhusu haki zao.

“Kampeni hii ya Mama Samia Legal Aid ni mkakati mahsusi wa Serikali wa kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anapata haki kupitia huduma ya msaada wa kisheria bila vikwazo vya kiuchumi,” amesema Msambazi.



Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA