BALOZI MAPURI:YATUMIENI VYEMA MAFUNZO MLIYOYAPA
- Get link
- X
- Other Apps
Na Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM.
MJUMBE wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Balozi Omar Ramadhan Mapuri amewataka watendaji wa uchaguzi kuhakikisha mafunzo waliyoyapata wanayawasilisha vyema kwa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata ili kuwawezesha kuratibu na kusimamia uchaguzi vizuri na kwa weledi.
Balozi Mapuri alitoa ombi hilo Jijini Dar es salaam Julai 23,2025 wakati akifunga mafunzo ya watendaji na wasimamizi wa uchaguzi kutoka mikoa ya Pwani na Dar es Salaam yaliyoanza Julai 21, 2025.
Amesema kupitia mafunzo waliyoyapata wanalojukumu la kuhakikisha wanayawasilisha kwa weledi ili wasimamizi hao ngazi ya kata waweze kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa
Pia Balozi aliwatahadhalisha
watendaji wa uchaguzi juu ya matumizi holela ya makundi Sogozi ya WhatsApp, na kuwataka kuyapunguza katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Octoba mwaka huu.
"Ni muhimu umuhimu kuwa na weledi, uaminifu na umakini katika utoaji wa taarifa kipindi hiki nyeti cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025"amesema
Aidha, amesema watendaji wa uchaguzi wana wajibu wa kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kwa lengo la kuwahabarisha wananchi na wadau wa uchaguzi.
Balozi Mapuri aliwaomywatendaji hao kuhakikisha taarifa zinazotolewa kwa vyombo vya habari zimesahihishwa na kujiridhisha kabla ya kuzitoa kwa umma, ili kuepusha taharuki isiyo ya lazima.
"Katika utekelezaji wa majukumu yenu mtapaswa kutoa taarifa mbalimbali kwenye vyombo vya habari ili kuwajulisha wananchi na wadau mambo mbalimbali ya uchaguzi.
Awali Mwenyekiti wa Mafunzo ya uchaguzi, Selemani Katetu aliipongeza INEC Kwa kuwawezesha kupitia mafunzo ya kina na ya vitendo katika nyanja mbalimbali.
"Katika mafunzo haya jumla ya mada 11 zilifudishwa kwa lengo la kuboresha uelewa na utendaji wa wasimamizi wa uchaguzi katika ngazi zote"amesema
Aidha amesema kupitia mafunzo hayo wameweza kujifunza utaratibu wa kuhesabu kura vituoni, kupiga kura pamoja na kupitia sheria za uchaguzi.
- Get link
- X
- Other Apps





Comments
Post a Comment