BENKI YA DUNIA KUJENGA MRADI WA NJIA YA KUSAFIRISHA UMEME WA KV 400 KUTOKA UGANDA HADI TANZANIA




Yakutana na Mhandisi Mramba kueleza kikao baada ya kujiridhisha kuwa matokeo ya kimazingira

Yaialika Wizara ya Nishati kushiriki Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa jijini New York

Mramba aahidi kuendelea na Benki ya Dunia miradi ya Nishati

Na Mwandishi wetu

BENKI ya Dunia (WB) imeeleza kuwa itatoa fedha za utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo mkubwa wa kilovolti 400 kutoka nchini Uganda hadi Tanzania.

Hayo, yameelezwa na Mtaalam wa Nishati kutoka Ofisi ya Benki ya Dunia nchini Tanzania, Dkt. Rhonda Jordan wakati alipofanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mha. Felchesmi Mramba katika Ofisi za Wizara ya Nishati Mji wa Serikali Mtumba Julai, 23 Jijini Dodoma.




Dkt. Rhonda amesema kuwa kwa sasa benki hiyo imeridhia kutekeleza mradi huo baada ya kujiridhisha kuwa matokeo ya kimazingira kama ilivyokuwa ikielezwa hapo awali.

“Bodi ya Wakurugenzi sasa itapitisha fedha kwa ajili ya kutekeleza mradi huo, ambao ulikuwa ukisuasua kutekelezwa kwa madai ya kuathiri mazingira, lakini sasa bodi imeridhika na itatoa fedha za kuanza kuutekeleza”, amesema Dkt. Rhonda

Katika hatua nyingine, Dkt. Rhonda ameialika Wizara ya Nishati kushiriki katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa utakaofanyika Jijini New York nchini Marekani mwezi Semptemba, 2025.

Katika mazungumzo yao, Katibu Mkuu Mramba amemueleza Dkt.Rhonda kuwa wataendelea na Benki ya Dunia katika miradi mbalimbali ya Nishati ikihusisha ule wa usafirishaji umeme wa Tanzania-Zambia (TAZA) na mingineyo inayofanya kazi kama hiyo.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mha. Innocent Luoga na Mhandisi Nishati Mkuu John Mageni.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA