DKT. NDUMBARO AIPA KONGOLE OCPD KWA KUTAFSIRI SHERIA 300



Na Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM 

WAZIRI wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro, amesema hadi kufikia Juni 30 mwaka huu  Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria (OCPD)kwa kutafsiri sheria 300 kati ya 446 kutoka lugha ya  kingereza kwenda lugha ya kiswahili.

Hivyo ameipongeza OCPD kwa kuweza kutafsiri Sheria hizo na kusisitiza Ofisi hiyo ni muhimu katika mustakabali wa Nchi.

Dkt Ndumbaro ametoa pongezi hizo alipotembelea katika Banda la (OCPD). lililopo katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es salaam (DTIF) yanayoendelea.




Amesema katika mwaka huu wa fedha Serikali imetega bajeti ili OCPD  iweze kutafsiri sheria 146 zilizobakia ili Sheria zote 446 ziwe katika lugha ya kiswahili ili watanzania waweze kuzielewa.

"Hii ndio kazi ya msingi ya Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria ...Ofisi hii ni muhimu sana katika mustakabali mzima wa kutunga na kuchakata sheria za nchi"amesema Dkt Ndumbaro 

Aidha amesema kuwa OCPD ni  muhimu katika mchakato mzima wa utunzi na urekebu wa sheria na kusisitiza kuwa bila Ofisi hiyo hakuna sheria inayoweza kwenda bungeni kutugwa .

Pia amesema bila OCPD hakuna sheria ambayo inafanyiwa marekebisho, na hakuna Sheria ndogo inatugwa 










Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA