FCC YAJIVUNIA KUTENGENEZA MAZINGIRA RAFIKI KWA WAWEKEZAJI
Na Mwandishi wetu
TUME ya Ushindani (FCC) imesema kupitia Serikali inajivunia kuweza kutengeneza mazingira rafiki ya wawekezaji ambayo yamewawezesha kupata fursa za ufanyaji biashara na kujiimarisha.
Hayo yamebainishwa Jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Nchini (FCC)khadija Ngasongwa alipotembelea Banda Tume hiyo katika maonesho ya 49 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea.
Amesema wawekezaji wa ndani ya nchi wamekuwa wakisimamiwa na sheria madhubuti zinazosimamia uwekezaji ili kusaidia kulinda na kuimarisha biashara zao.
"Lengo la kuanzishwa kwa Tume ya Ushindani(FCC) ni kusimamia na kuhimarisha ufanyaji wa biashara nchini, kulinda walaji dhidi ya mienendo potofu ya hali ya ufanyaji biashara kati ya kampuni na kampuni,pamoja na kudhibiti bidhaa bandia."amesema Ngasongwa
Amesema lengo kubwa ni kuhakikisha wawekezaji ndani ya nchi waweze kutambua kuwa kuna sheria madhubuti ambazo zitawalinda na kusimamia uwekezaji wao wanaoufanya.
Ngasongwa amesema FCC itaendelea kutimiza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha hali ya biashara Nchini.
Akizungumzia kuhusu maonesho ya 49 kimataifa ya biashara yanayoendelea amesema ushiriki wao
katika maonyesho hayo ni fahari kubwa,huku akiwaomba wageni wanaopita kwenye maonyesho hayo kuchangamkia fursa za uwekezaji.
Amesema kuwa Kwa upande wa mwekezaji Mwenye mtaji mdogo anaweza kupata fursa kuungana na mwekezaji mwenye kipato kikubwa au mwenye uwekezaji mkubwa na kuweza kuhimarisha biashara kwa pamoja.


Comments
Post a Comment