GCLA YAWAITA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LAO SABASABA



Na Mwandishi wetu

MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA)imewakaribisha wananchi kutembelea katika Banda lao lililopo katika Maonesho 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba(DIFT)  ili waweze kupata elimu ya masuala mbalimbali hasa katika masuala ya kemikali.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Huduma za Uchuguzi wa Mazingira, Dkt Peter Shimo wakati akizugumza na waandishi wa habari katika maonesho hayo yanayoendelea.

Amesema lengo la GCLA ni kuhakikisha jamii inapata elimu ya kemikali na mambo mengine yanayohusiana na mamlaka katika maeneo yote.

"Huduma tunazozitoa hapa ni pamoja na za usajili wa kemikali,wahusika wanaofika hapa pia wanapata elimu kuhusu shughuli zetu pia tunasajili wajasiriamali wanaojihusisha na masuala ya kemikali,"amesema Dkt Shimo




Aidha aliwaomba wajasiriamali wanaojishughulisha na kemikali kufika katika Banda lao ili kuweza kupata elimu kuhusu kemikali pamoja na kufanya usajili wa bidhaa hiyo

"Wajasiriamali watakaotembelea banda letu ambao wanajishughilisha na shughuli za kemikali bila usajili pia watapewa maelekezo ya taratibu zakufuata ili kukamilisha usajili" amesema 

Ameongeza kuwa mamlaka hiyo ina mfumo wa kusajili wajasiriamali mtandaoni kwa ajili ya watu ambao wapo mbali na watoa huduma hiyo.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA