HAYA NDIYO BAADHI YA MAFANIKIO MAKUBWA YA CCM KWA VIJANA.

 





Na Mwandishi wetu 

KATIKA Ilani ya Uchaguzi wa 2020–2025 na ile ya 2025–2030, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeweka wazi dhamira ya dhati ya kuwekeza kwa vijana.

Dhamira hiyo ni pamoja na kujumuisha ajira kwa vijana ambapo zaidi ya ajira milioni 8.08 zimetengenezwa kati ya mwaka 2020 hadi 2024.

Pia mikopo ya Elimu ya Juu kwa Wanafunzi 245,799 ambao wameweza kupata mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka 2024.

Vilevile elimu bila malipo kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha sita iliyotolewa bila ada, ikiwa ni sehemu ya mzigo kwa wazazi na kulea taifa la wasomi.




Pia Samia Scholarship ambapo Jumla ya wanafunzi 3,696 wamefadhiliwa kusoma sayansi, tiba na uhandisi kupitia ufadhili wa Rais Samia.

Huku Mikopo kwa Vijana Shilingi bilioni 96.3 zimetolewa kwa vijana 8,242 kupitia halmashauri mbalimbali kwa ajili ya shughuli za kiuchumi.

Katika eneo la TEHAMA na Ubunifu CCM inapanga kuandaa soko la ajira la kisasa kwa vijana katika TEHAMA, start-ups, na mafunzo ya stadi za kidigitali.

Huku upande wa Michezo na Sanaa, Samia Youth Art Fund na kuwekeza filamu kwenye viwanja vya vimefungua milango kwa vijana wenye vipaji katika muziki, mitindo na michezo.




Kwa upande wa wanasiasa za vijana kwa sasa ni mabalozi wa Demokrasia.

Ambapo CCM imefanya maboresho ya kanuni zake Machi 2025 ushiriki mpana wa vijana.

 Katika uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 2024, zaidi ya asilimia 60 ya walioshinda walikuwa vijana. 

Hii ni ishara kuwa vijana hawasubiri kupangiwa tena, bali wanajitokeza na kuaminiwa na wananchi.

Huku ukomo wa viti maalum kwa wanawake umeongeza ushiriki wa vijana wanawake, jambo linaloimarisha usawa wa kijinsia na wajibuji.


Chini ya Uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, vijana safu wa mbele katika ajira, elimu, diplomasia, sanaa na michezo. 

Kauli mbiu yake ya “Kazi na Utu, Tunasonga Mbele” si maneno tu, bali ni dira ya kweli ya maendeleo.

Rais Samia ameanzisha fursa nyingi zinazowalenga vijana, akiwemo Rais wa kwanza mwanamke kuwateua vijana wengi katika nafasi za uongozi wa juu serikalini.


Chama cha Mapinduzi (CCM) ni chama makini, chenye misingi imara na maono ya mbali. 

Ni chama pekee kinachotambua kuwa taifa linalojenga vijana leo lina uhakika wa viongozi bora kesho. 

Ni wakati wa vijana kujitokeza kwa wingi, chukua fomu, kushiriki katika siasa, na kusaidia kuwa sauti yao inasikika kwenye kichwa cha taifa.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA