INEC YAENDELEA KUTOA MAFUNZO KWA WARATIBU NA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI

 



Na Mwandishi wetu

MJUMBE wa Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Omar Ramadhan Mapuri, amewataka watendaji wa uchaguzikati ukizingatia wanafuata taratibu mbalimbali ili kuondoa vurugu zinazoweza kutokea katika mchakato wa uchaguzi.

Balozi Mapuri ametoa ombi hilo mapema leo Julai 21, 2025, mkoani Dar es Salaam wakati akifungua mafunzo kwa watendaji wa uchaguzi wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.




Amesema Mafunzo hayo yanahusisha waratibu wa uchaguzi, wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wa uchaguzi wa ngazi ya jimbo, mamlaka ya uchaguzi pamoja na mamlaka ya ununuzi yanatarajiwa hadi Julai 23, 2025.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume hiyo, Giveness Aswile, amesema mafunzo hayo yalipangwa kwa awamu mbili, ambapo awamu ya kwanza yalifanyika Julai 15 hadi 17, na awamu ya pili ya kuanzia Julai 21 hadi 23 mwaka huu.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA