INEC YATOA WITO KWA MAKUNDI YA KIJAMII KUAMASISHA USHIRIKI WA WANANCHI KATIKA UCHAGUZI MKUU 2025



Na Mwandishi wetu

TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imeyataka makundi mbalimbali ya kijamii nchini kuyatumia majukwaa yao kuwahamasisha wananchi kushiriki kwa wingi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Wito huo umetolewa leo, tarehe 31 Julai 2025, jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Mheshimiwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele, wakati akifungua mkutano kati ya Tume na wawakilishi wa watu wenye ulemavu.

Jaji Mwambegele ameeleza kuwa Tume inatambua na kuthamini mchango wa watu wenye ulemavu katika kueneza taarifa sahihi na kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika uchaguzi.




“Nawasihi kutumia majukwaa yenu kuhimiza wenzenu kushiriki kwa amani na kuepuka kauli au vitendo vinavyoweza kuhatarisha utulivu wa nchi yetu wakati wa kampeni,” amesema Mwambegele, na kuongeza kuwa Tume itaendelea kushirikiana nao katika hatua zote muhimu kuelekea uchaguzi.

Akizungumzia maandalizi ya uchaguzi mkuu, Jaji Mwambegele amesema kuwa ratiba rasmi imeshatangazwa ambapo utoaji wa fomu za uteuzi kwa wagombea wa nafasi mbalimbali utafanyika kuanzia tarehe 9 Agosti hadi 27 Agosti 2025, huku kampeni zikipangwa kuanza tarehe 28 Agosti hadi 28 Oktoba 2025 kwa upande wa Tanzania Bara.


 

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA