JESSICA : CCM INAJALI UONGOZI WA VIJANA

 



Na Mwandishi wetu

KATIBU wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM TAIFA, Jessica Mshama amesema Chama Cha Mapinduzi kinajali sana uwezo wa Vijana katika uongozi ndio maana kinawaamini na kuwapa nafasi za juu za kiuongozi.

Jessica Mshama aliyasema hayo wakati wa mahojiano na Watangazi wa Kipindi cha Sentro cha Clouds Tv kilichofanyika 8, 2025 katika studio ya Clouds Tv Jijini Dar es Salaam.


Jessica ameonesha uthabiti wa CCM katika uongozi wake kwa kuitofautisha na vyama vingine kutokana na kuwaamini Vijana katika nafasi mbalimbali za kiuongozi na kwamba ushindi wa CCM hautokani kwa bahati mbaya kwa sababu kimejenga zaidi kwa Vijana.





Kuhusu suala la Uchaguzi, Jessica Mshama amesema kuwa Viongozi wa Juu wa Jumuiya ya UVCCM wamekuwa wakiratibu Mikutano inayohusisha Ziara zao katika Mikoa mbalimbali kwa ajili ya kuhamasisha Vijana kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali pamoja na kujiandaa kupiga kura ifikapo Oktoba 2025.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA