KASI YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UMEME JUA KISHAPU, WAMKOSHA BALOZI WA UFARANSA

 


Na Mwandishi wetu

BALOZI wa Ufaransa Nchini Tanzania Anne Sophie Ave ametembelea na kukagua Mradi wa umeme wa Jua (solar) uliopo Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga na kujionea kasi kubwa ya maendeleo ya utekelezaji wa Mradi huo ambao mpaka sasa umefikia asilimia 67.

Mazungumzo katika ziara Juni 27,2025 Balozi amesema kuwa ziara hiyo ni kuona mipango hiyo ya maendeleo ya Tanzania ambayo inafadhiliwa na umoja wa Nchi za ulaya na shirika la Maendeleo la Ufaransa.

“Sababu kubwa ya mimi kuja hapa, ni kutaka kujionea miradi ya maendeleo ambayo Umoja wa Nchi za Ulaya na Shirika la maendeleo ya Ufaransa inaifadhili, ikiwa ni mradi huu wa uendelee umeme wa jua hapa Kishapu, nimeona tija ya mradi huu kwa wananchi lakini pia nimeona thamani ya pesa ambayo tumeitoa, kazi ni nzuri na watendaji hapa wanafanya kazi kwa bidii na kujitoa sana, niwaombe waendelee kufikisha mradi huu wa Balozi.



Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Peter Masindi Amesema kupitia ufadhili wa Umoja wa Maendeleo ya Nchi za Ulaya na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD)Kiasi cha Shilingi Bilioni 323 kimetumika katika kutekeleza Mradi wa umeme utakaozalisha Megawati 150 na kuwataka Watanzania wakae tayari katika kuutumia Ume huo kwa maendeleo ya uchumi wao na wataifa kwa ujumla.

Naye Mkurugenzi Wa Miradi TANESCO, Mhandisi Timothy Mgaya Amesema kuwa Umoja wa Nchi za Ulaya na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) umefadhili miradi mbalimbali ya umeme kupitia Serikali ya Tanzania ikiwa ni pamoja na Mradi wa Kakono, Mradi wa kuinganisha Tanzania na Zambia (TAZA), Mradi wa kuiunganisha Tanzania na Uganda pia imeonesha nia ya kuendelea kuifadhili miradi mingine ya Umeme.



Ameishukuru Serikali kuendelea kuwekeza kwenye miradi ya umeme itakayowezesha kuwepo kwa umeme wa uhakika na hivyo kuiwezesha Tanzania kutekeleza mkakati wa matumizi ya nishati safi ya umeme.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA