UWT ILALA YAWAITA WANAWAKE KINYANG'ANYIRO CHA UDIWANI UBUNGE .
Na Mwandishi wetu
KATIBU wa Umoja wa Wanawake(UWT) Wilaya ya Ilala, Rosemary Mwakisalu amewasihi Wanawake Wilayani humo kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kugombea Ubunge na Udiwani.
Mwakisalu ametoa rai hiyo Julai 1,2025 wakati. na Waandishi wa habari mwendo wa zoezi la uchukuaji wa fomu za kugombea nafasi za uongozi wa chama hicho.
"Natoa wito kwa Wanawake wote wa Ilala, wajitokeze kwa wingi kuchukua fomu, na gharama yetu ya fomu ni shilingi 50,000 tu hakuna mchango unaotolewa"amesema Rosemary.
Aidha amesema kwamba tangu kuanza kwa zoezi la uchukuaji wa fomu Juni 28,2025 ,Wanawake wameendelea kujitokeza kwa wingi katika Wilaya hiyo kuchukua fomu kwa nafasi mbalimbali.
"Mpaka dhana Juni 30,2025, jumla ya wanawake wapatao 63 walikua wamechukua fomu kugombea nafasi ya Udiwani Viti maalumu Wilaya ya Ilala,nafasi za kata Wanawake wapatao 52 walikua wameshajitokeza kuchukua fomu kugombea Udiwani wa kata."amesema
Kwa upande wa nafasi ya Ubunge wa Majimbo amesema toka Juni 30,2025 Wanawake wapatao 10 wamejitokeza nafasi ya Ubunge wa Majimbo.
Aliwapongeza wanawake na kuwataka kuendelea kujitokeza kuomba nafasi hizo
.

Comments
Post a Comment