LUKUVI AIPONGEZA WIZARA YA NISHATI KUTEKELEZA AZMA YA SERIKALI YA KUHAMIA KATIKA MJI WA SERIKALI MTUMBA

 


Aishukuru Wizara kwa kumheshimisha Dkt.Samia Suluhu Hassan

Ampongeza Dkt. Biteko kwa kuweka msukumo wa Watumishi kuhamia Mtumba

Na Mwandishi wetu

WIZARA ya Nishati imeongezwa kwa kuhamia rasmi katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma ambapo Idara na Vitengo vyote vya Wizara sasa vimeshahamia katika jengo la Wizara lililopo katika Mji huo wa Serikali.

Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu, William Lukuvi wakati alipotembelea jengo la Wizara katika Mji wa Serikali Mtumba ambapo alipokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, Naibu Katibu Mkuu, Dkt. James Mataragio pamoja na Menejimenti ya Wizara.

"Nakupongeza sana Katibu Mkuu kwa hatua hii, pamoja na Mkandarasi wa Jengo na Msimamizi, pia nawapongeza kwa nia thabiti ya kuhamia katika Mji huu wa Serikali baada ya Mhe. Rais Samia kutoa fedha zilizowezesha ujenzi wa majengo haya Serikali Mtumba". Amesema Lukuvi




Ameongeza kuwa, nia ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ni wananchi wanaopata huduma kwa ufanisi katika ufanisi na hivyo kuondoa kutumia eneo moja muda mrefu kupata huduma katika maeneo tofauti.

' Nawashukuru sana Wizara kwa kumshangaza Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa sababu nia yake ni Watumishi kuwa katika utoaji huduma ili kuleta ufanisi.” Amesema Lukuvi

Amempongeza pia Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko kwa kuweka msukumo kwa Wizara katika kukamilisha jengo hilo na watumishi kuhamia katika jengo husika.

Aidha Lukuvi ametoa rai kwa watumishi wa Wizara kusaidia wanatunza vyema na vifaa vilivyotumika ili viweze kudumu kama ilivyokusudiwa.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA