Mto wachepushwa ili kujenga tuta la kufulia Umeme Kasi yapamba moto kukamilisha Mradi Na Mwandishi wetu UJENZI wa Mradi wa Bwawa la kufua umeme kwa maji kupitia mto Malagarasi (MW49) umefikia hatua muhimu, kwa kuweza kuchepusha maji ya kwenye mto (kutengeneza njia ya maji) ili kuruhusu ujenzi wa Tuta kuu,litakalotumika katika kufua umeme. Akizungumza katika hafla fupi ya uchepushaji maji, Agosti 13,2025 Meneja wa Mradi Mha. Saidi Kimbanga amesema kuwa hatua hiyo ni muhimu katika utekelezaji wa mradi huo ambao kwa sasa ujenzi wa mradi umefikia kwa Asilimia 10, na unatarajia kukamilika mwanzoni kwa mwaka 2027. “Ujenzi wa mradi unaenda kwa kasi sana, uchepushaji maji ulitakiwa kufanyika tarehe 27, mwezi huu, lakini tumefanikisha zoezi hili leo, siku zaidi ya kumi nyuma, hivyo tunatarajia hata mradi utakamilika mapema zaidi” alisema Saidi Akizungumzia umuhimu wa uchepushaji maji, Saidi amesema kuwa maana nzima ya ujenzi wa Bwawa la kufua umeme unahitaji kuweza kudhibiti maji ili yaweze kup...
Comments
Post a Comment