MATUMIZI YA UMEME KIGOMA YAONGEZEKA
Ni uhusiano na Gridi ya Taifa ya umeme
MD Twange nawahakikishia wana Kigoma kupata umeme wa uhakika
Na Salama Kasamalu, KIGOMA
MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Lazaro Twange amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mheshimiwa Simon Siro, tJulai,2 2025 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambapo amesema kwamba umeme Mkoa wa Kigoma ni ushahidi wa mahitaji makubwa ya umeme Mkoani humo.
Ongezeko hili linafuatia kuunganishwa kwa Mkoa wa Kigoma katika Gridi ya Taifa ya umeme Disemba 2024. Matumizi ya umeme yameongezeka kutoka Megawati 17 hadi kufikia Megawati 24.
“Ongezeko hili linaonesha kwamba kulikuwepo na uhitaji mkubwa wa umeme katika Mkoa wa Kigoma. Kuunganishwa kwa Mkoa huu na Gridi ya Taifa lazima mabadiliko chanya”, alieleza Twange.
Aidha, alimhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa TANESCO iko tayari kutuma ujumbe kupitia ujumbe unaojitokeza kwa wakati, ili kuhakikisha huduma ya umeme iko bila kuwapo.
"Niwahakikishie wakazi wa Kigoma kuwa TANESCO itaendelea kupata upatikanaji wa umeme na uhakika kwa ajili ya shughuli za kilimo, biashara na matumizi ya majumbani," amesema Twange.
Pia, katika kuunga mkono mkono wa Serikali ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, Twange alikabidhi majiko ya umeme kwa familia ya Mkuu wa Mkoa Simon Siro pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye na kuwaomba watumie vifaa hivyo kama mfano wa jamii.
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mtendaji alitembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Kufua Umeme wa Malagarasi (MW 49.5) pamoja na Kituo cha Kupooza Umeme cha Kidahwe. Alieleza kuwa TANESCO inaendelea kumsimamia mkandarasi ili kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati uliopangwa.
“Ninamshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa zaidi ya Shilingi Bilioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa mradi huu wa Malagarasi.
Ziara ya Mkurugenzi Mtendaji inalenga utekelezaji na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya TANESCO katika mikoa ya Kanda ya Magharibi, ikiwa ni pamoja na Mkoa wa Kigoma.





Comments
Post a Comment