MFANYABIASHARA CHACHA NCHAMA AJITOSA UBUNGE JIMBO LA KIVULE
Na Mwandishi wetu
MFANYABIASHARA Chacha Nchama amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge Jimbo la Kivule kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Nchama amechukua fomu hiyo leo Julai 1,2025 kwa Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala Sylvester Yaredi.
Aidha amesema kwamba ametia nia ya kugombea nafasi hiyo kwa lengo la kumsaidia Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuondoa changamoto zinazokabili Jimbo la Kivule.


Comments
Post a Comment