MFANYABIASHARA MAARUFU 'RAIS WA SINGIDA' AJITOSA UDIWANI KATA YA KIVULE
Na Mwandishi wetu
MFANYABIASHARA wa kusafirisha mizigo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Simon Ititi maarufu Rais wa Singida amechukua fomu hii kugombea udiwani Kata ya Kivule.
Ititi ameichua fomu ya kuomba ridhaa kugombea nafasi hiyo katika ofisi za CCM Kata ya Kivule na kurudisha huku akiweka wazi dhamira ya kugombea nafasi hiyo ya uongozi.
"Mimi ni Mkazi wa Kivule, najua adha wanayokutana na wananchi wa Kivule kusababisha kuzorota kwa Uchumi wa mwananchi mmoja mmoja.
" Kivule Kuna changamoto nyingi lakini kubwa inayoninyima usingizi na kunishawishi kugombea ni miundimbinu ya barabara si rafiki.
"Barabara haipitiki wakati wote na wakati wa mvua ndio haipitiki kabisa hali inayosababisha gharama za usafiri kupanda,"anasema Ititi.
Amesema amedhamiria nafasi kutumia hiyo kwa weledi mkubwa ili kukidhi haja za wananchi wa Kata ya Kivule




Comments
Post a Comment