MTEI MCHORAJI RAMANI ZA MAJENGO ASIYE MIKONO
Na Mwandishi wetu
KIJANA Joseph Mtei Mwanafunzi wa mwaka wa pili kutoka Chuo cha Elimu na Ufundi Stadi (VETA) Dodoma amekuwa akichora ramani za majengo za kila aina kupitia miguu yake.
Mtei yupo kwenye Maonesho 49 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba, yaliyopo Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mtei ambaye ni mlemavu wa mikono amesema anasomea masuala ya uchoraji wa ramani na sasa anauwezo wa kuchora ramani ya aina yoyote.
"Naipenda VETA kwa kunikubalia kujiunga kwa ajili ya ujuzi huu, kwasababu hawakuona kwamba mimi ni mlemavu ambaye sina mikono labda nitakua mzigo kwa walimu walinichukulia kama wanafunzi wengine,"amesema.
Amesema alijiunga na VETA Mwaka wa kwanza 2024 na sasa yupo mwaka wa pili,huku akiwa na uwezo wa kuchora ramani yoyote popote pale.
Mtei amesema ili ramani ikamilike imekuwa ikitumia zaidi wiki moja na si kwa siku moja
Aidha Mtei kutumia fursa hiyo kuomba
jamii kuacha kuwaficha watu wenye ulemavu nabadala yake wapeleke VETA wapate ujuzi utakaosaidia kujikwamua kiuchumi.

Comments
Post a Comment